Yanga sasa itacheza kombe la shirikisho Afrika baada ya kuondolewa kunako ligi ya vilabu bingwa Africa, kanuni za CAF katika round hii ya 16 ni kwamba timu 16, ambazo hazikufuzu hatua ya makundi klabu bingwa zitakutanishwa na timu 16, zilizofuzu hatua ya kwanza michuano ya kombe la Shirikisho na droo itafanyika siku ya jumatano.
Kanuni pia za CAF zinasema timu iliyotolewa klabu bingwa ndio itakua mwenyeji wa mechi ya kwanza katika mzunguuko huo wa mtoano na mechi zinatarajiwa kuchezwa kati ya Aprili 6 na 8.
Tayari timu 16 zilizofu hatua ya play off katika michuano hii ambazo moja wapo ndio itapangiwa kucheza na Yanga zimeshajulikana baada ya michezo ya mwishoni mwa juma.
Moja ya timu hizi ndio itapangiwa kucheza na Yanga SC
1. Cara Brazzavile-Congo
2. Welayta Dicha-Ethiopia
3. Al Masry- Misri
4. Akwa United-Nigeria
5. Enyimba-Nigeria
6. Djoliba Ac-Mali
7. Costa Do Sol-Mozambique
8. Hilal Obayed-Sudan
9. USM Alger-Algeria
10. Supersport United- Afrika kusini
11. CS La Mancha -Congo
12. CR Beleuzdad -Algeria
13. RSB Berkane -Morroco
14. Fosa Junior-Madagascar
15. Raja Casablanca-Morocco
16. Deportivo Niefang-Equatorial Guinea.
Kati ya timu hizo hapo moja wapo ndio itakuwa mpinzani wa Yanga baada ya draw ya jumatano saa 8:30 mchana jijini Cairo.