Nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto akivaa medali ya mshindi wa pili ya Kombe la Shirikisho Afrika
Shirikisho Afrika

Yanga: Hatuna Wachezaji Wadogo, Sisi Ndio Tumefanikiwa Zaidi.

Sambaza....

Baada ya kurejea nchini wakitokea Algeria katika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika walilipoteza ubingwa huo Yanga wamesema wao ndio mfano wakuigwa ukanda huu wa Cecafa.

Rais wa Yanga Hersi Said akitoka kuiongoza Yanga kucheza fainali yake ya kwanza kubwa Afrika ameongea katika kipindi cha asubuhi cha Wasafi Fc na kusema “ Sisi ndiyo timu iliyofanikiwa zaidi katika Ukanda wetu wa CECAFA. Timu nyingine zinapaswa kuja tuzifundishe jinsi ya kusajili vizuri wachezaji, jinsi ya kushinda mataji, jinsi ya kujiendesha, tuna mfumo mzuri na zije kujifunza jinsi ya kuwaamini wachezaji vijana.”

Hersi pia aliuongelea mchezo wa fainali na kutoa faida za kuwa na wachezaji wazoefu katika michuano hiyo mikubwa namba mbili kwa ngazi za klabu Afrika. Si hayo tu pia Rais huyo aligusia pia katika mkataba wa kocha Nabi na Fiston Mayele ambao wanatajwa kutimka Yanga.

Baadhi ya viongozi wa Yanga.

“Kama tungekuwa na wachezaji wadogo katika ile mechi ya USM Alger ingeweza kuwa dhahama kwetu, lakini uzoefu wa mtu kama Diarra umetusaidia kwa kiasi kikubwa. Sisi tuliokuwa jukwaani ndiyo tulikuwa tunaogopa, lakini wachezaji wenyewe kiwanjani hawakuwa na wasiwasi,” alisema Hersi na kuongeza “Kocha Nabi tunae sana, wakala wake ni mtoto wake na tulikuwa nae katika safari ya Algeria na yuko mjini hivi sasa. Amekuja kwa ajili ya kuijadili mkataba mpya ambao ule wa zamani unamalizika mwishoni kwa msimu huu”

“Tunajivunjia mchezaji wetu kutakiwa na timu zote kubwa za Afrika. Ingeshangaza tufanye vizuri alafu isiwe kocha wala mchezaji wetu kutakiwa na timu nyingine,” alimalizia Hersi.

Yanga sasa wanarudi nchini na kuendelea na michuano ya ndani ambapo wana michezo miwili katika Ligi na mchezo mmoja wa fainali ya Kombe la FA.

 

Sambaza....