Ligi Kuu

Ndanda dhidi ya Simba SC

Sambaza....

Bila shaka utakuwa mchezo wenye ushindani mkubwa hasa kwa kuzingatia nafasi katika msimamo wa ligi, na uhitaji wa alama tatu ni changamoto kubwa kuelekea katika mchezo wa leo. Ndanda fc wapo nafasi 11 wakiwa na alama zao 11 hivyo wataingia katika mchezo wa leo kusaka alama tatu muhimu kwao ili kujiweka katika mazingira mazuri

Kwa upande wa Simba sc wapo kunako nafasi ya pili wakiwa na alama 23 hivyo wakihitaji alama tatu katika mchezo huo ili kuendelea kushika usukani wa ligi

Ndanda fc wao hupendelea zaidi mifumo ya 4-4-2 au 4-5-1 na kwa line up iliyotoka bila shaka watatumia mfumo wa 4-5-1 lakini kubwa Ndanda wapaswa kuwa makini sana na aina ya uchezaji wa Simba hasa kwenye eneo la kiungo, mahala ambao mara hutumika kuamua mchezo

Ndanda wanatakiwa kuziba njia zote ambazo Simba hutumia kupitisha mipira yao, ili kuwalazimisha watumie zaidi square passes ambazo mara nyingi zinakuwa hazina madhara

Lazima wahakikishe wanafanya halfway offensive ili kukataa kujilinda moja kwa moja, huku wakiongeza umiliki wa mpira kwenye final third ya Simba ili kutafuta faulo ambazo wakizitumia vizuri zinaweza kuwasaidia kupata bao

Kwa aina ya washambuliaji wao long balls zinaweza zisiwe na faida kwao kwa maana ya kukosa mtu sahihi wa kupokea aina hiyo ya mipira na kujikuta wanapoteza mingi na automatically kujikuta wakicheza mchezo wa kujilinda muda wote

Kwa upande wa Simba sc hawa ni wazuri sana kwenye kumiliki mpira, pressing na cutoff wana viungo wengi wenye skills nzuri sana

Kwa line up iliyotoka bila shaka watatumia mfumo wa 4-3-3 yani walinzi wanne nyuma Paul Bukaba kulia na Erasto nyoni kushoto James kotei na Juuko murshid kama walinzi wa kati, hapa ni wazi msingi mkuu wa mashambulizi ya Simba yataanzia kwa hao watu wa nne wa chini

Viungo Jonas mkude, Mzamir Yasin na Mohammed Ibrahim hawa watatakiwa kuijenga timu katika pattens zote (offensive patterns na defensive patterns) wakiwa na majumu ya kuwalisha mipira Shiza kichuya, John bocco na Juma Luizio

Huu ni mfumo ambao unahitaji kuwa na viungo washambuliaji zaidi ya mmoja (unconventional formation) hapo unaweza kumuona Mo Ibrahim akichezesha timu kama holding na passer huku Mzamir Yasin akibaki kuwa deception plan kama invisible attacking midfield huyu ndiye kiungo wa juu akicheza pamoja na Jonas mkude na anaweza kuwaumiza Ndanda kwenye second balls na counter endapo tu tactical screening kutoka kwa Mo Ibrahim na Shiza kichuya zitafanyika vizuri.

Sambaza....