La Liga

Ni derby ya Madrid katika vita ya kuwania nafasi

Sambaza....

 

Leo kuna derby nyingine pale Hispania kunako ligi kuu ya nchini humo maarufu kama La Liga, ambapo Real Madrid watakuwa nyumbani Santiago Bernabeu kuwakaribisha wapinzani wao wa jadi Atletico Madrid

Licha ya kuwa ni wapinzani wa jadi, lakini vita kubwa katika derby hii ni kuwania kumaliza kunako nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo, hivyo kutofautiana na ile tuliyoishuhudia jana kati ya Manchester City dhidi Manchester United

Real Madrid wapo katika nafasi ya tatu wakiwa na 63, baada kushuka dimbani mara 30, huku Atletico Madrid wakiwa kunako nafasi ya pili kwa alama zao 67, wakishuka dimbani mara 30, pia

Atletico Madrid wataingia katika mchezo huu wakiwa hawana rekodi nzuri ya kushinda kunako uwanja wa Bernaneu, tangu walipofanya hivyo mwaka 2016 walipopata ushindi wa bao 1-0, huku wakishinda michezo minne kati ya 11, ya ligi derby chini ya kocha Diego Simione “El chollo”

Katika michezo minne iliyopita ya ligi hiyo Atletico wameshinda michezo miwili, wakishinda mabao 2-0 dhidi Sporting CP, baada ya kutoka kuibamiza Derpotivo La Coruna bao 1-0 hivyo inaweza kuwa ni hamasa kwao kuelekea katika mchezo wa leo

Lakini pia Real Madrid wanaonekana kuimalika sana kwa sasa kunako ligi hiyo, wakishinda michezo 12, katika michezo yao 14, iliyopita ya ligi hiyo

Real Madrid haijapoteza mchezo tangu Februali 27, 2018 walipofungwa bao 1-0 na Espanyol, huku wakichagizwa na ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Juventus katika michuano ya Ulaya

Kumaliza kunako nafasi ya pili katika ligi hiyo inaweza kuwa ni changamoto nyingine kwa kocha Zinidine Zidane, ya kumfanya aendelee kuaminika kunako viunga vya Wafalme hao wa Madrid

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x