Sambaza....

Kamati ya utendaji ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), imemteua Ndg Athuman Nyamlani kuwa kaimu Makamu wa Rais wa shirikisho la hilo

Nyamlani anachukua nafasi ya Michael Richard Wambura aliyefungiwa maisha na kamati ya maadili kutojihusisha na masula ya mpira, Ingawa Michael Richard Wambura amekata rufaa katika kamati ya Rufaa ya TFF

Kwa mjibu wa Kanuni na Taratibu za TFF mtu ambaye anatakiwa kukaimu nafasi ya Uongozi kwa nafasi ya kuchaguliwa anatakiwa kuwa ni mjumbe wa muda mrefu wa TFF ambaye yupo kwenye kamati tendaji, kwa wajumbe wa kamati tendaji ambao wana muda mrefu kwenye Shirikisho kwa sasa ni watatu ambao ni Athumani Nyamlani, Msafili Mgoyi na Khalid Mohammed

Kikao cha kamati tendaji kilichofanyika jana jijini Dar es salaam, kilishidwana kwenye kumpitisha Athuman Nyamlani kukaimu nafasi hiyo ndipo kura za Ndio na hapana zikapigwa na kura za Ndio zikawa nyingi akapitishwa Athuman Nyamlani kuwa kaimu Makamu wa Rais wa TFF mpaka pale mkutano mkuu utakapofanya maamuzi mengine

Sambaza....