Uhamisho

Nyota wa Kagera Sugar Atimkia Ubelgiji

Sambaza....

Mshambuliaji wa “Wanankurukumbi” Kagera na timu ya Taifa Tanzania “Taifa Stars” Anuary Jabir ameondoka nchini na kwenda nchini Ubelgiji katika klabu ya KAA Gent.

Anuary Jabir atakua nchini humo kwa muda wa wiki mbili akipata mualiko wa kufanya majaribio katika klabu ya KAA Gent inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Ubelgiji maarufu kama Pro League.

 

Klabu yake ya Kagera Sugar tayari imeshatoa taarifa rasmi na kumtakia kila lakheri mshambuliaji huyo ambae alikuepo katika kikosi cha Stars kilichocheza michezo miwili ya kufuzu Afcon dhidi ya Uganda licha ya kukosa nafasi yakucheza.

“Mshambuliaji mwenyewe Anuary Jabir amepata mualiko wa wiki mbili kutoka klabu ya Ligi Kuu ya Ubelgiji (Belgium Pro League) KAA Gent kwaajili ya majaribio yakuchezea timu hiyo. Klabu inamtakia kila lakheri na kumuombea mafanikio katika majaribio hayo,” ilisema taarifa ya klabu.

Anuar Jabir (kulia) akiwa katika mazoezi ya Timu ya Taifa

Anaury Jabir mchezaji wa zamani wa Dodoma Jiji mpaka sasa ana mabao manne na pasi moja ya bao katika michezo ya Ligi Kuu ya NBC. Akifanikiwa katika majaribio yake ataungana na Watanzania wengine wanaosakataka kandanda nchini Ubelgiji kina Mbwana Samatta, Kelvin John na Novatus Dismas.

Sambaza....