Baadhi ya wachezaji wa Yanga wakiwa na kocha wa viungo
Uhamisho

Mwingine Atimka Yanga na Kutua Afrika Kusini

Sambaza....

Aliyekua kocha wa viungo wa Yanga Helmy Gueldchi ametimkia nchini Afrika Kusini na kujiunga na wababe wa Soweto Orlando Pirates.

Gueldich anaesifiwa kwa uandaaji mzuri wa wachezaji wa Yanga katika kipindi cha miaka miwili ambapo mara mbili wa Yanga ilitwaa mataji  matatu chini ya Nasreddine Nabi na amekuwa akihitajika sana tangu aondoke kwenye klabu hiyo.

Alikuwa sehemu ya wafanyikazi wa ufundi ambao Nabi alikuwa akilenga kwenda nao endapo angepata kazi mpya baada ya mazungumzo ya awali na Kaizer Chiefs ambayo hayakufanikiwa.

Kwa mujibu wa mtandao wa Idiski Times Helmy imekua rahisi kwake kuhamia kwa Maharamia hao baada ya kocha Nasraddine Nabi kupata kibarua kipya nchini Morocco alipojiunga na AS FAR.

Aliyekua kocha wa viungo wa Yanga Helmy pamoja na Kenedy Musonda.

Vyanzo vya habari ndani ya kambi ya Buccaneers vimethibitisha kuwa alisaini mkataba wa kujiunga nao kabla ya msimu mpya na ameanza mchakato wake wa kupata kibali cha kufanya kazi na kukimbia kabla ya kuhamia Afrika Kusini rasmi.

Gueldich ana uzoefu mkubwa katika bara zima na huku Pirates ikirejea Ligi ya Mabingwa ya CAF msimu huu, bila shaka utaalamu wake utakuwa nyongeza kubwa kwa timu yao ya ufundi kabla ya kampeni inayotarajiwa kuwa ngumu na kutwaa mataji matano.

Sambaza....