Saidoo Ntibazonkiza
Stori

Saidoo Ntibazonkiza Kiungo Bora wa Msimu!?

Sambaza....

Msimu wa Ligi Kuu ya NBC 2022/2023 unaelekea kumalizika huku ikiwa imebaki mizunguko miwili kwa Ligi hiyo kumalizika na kama ilivyo ada ni wakati sasa kukuwatambua na kuwakuwapongeza waliofanya vyema.

Miongoni mwa tuzo ambazo hutolewa ni pamoja na mfungaji bora, kipa bora, beki bora, mchezaji bora chipukizi, mchezaji bora wakigeni pamoja na kiungo bora ambayo kwangu mimi anastahili Saidoo Ntibazonkiza kiungo mshambuliaji wa Simba.

Saido alianza msimu akiwa na Geita Gold aliyojiunga nayo baada ya kuachana na Yanga na wakati wa usajili wa dirisha dogo akajiunga na Wekundu wa Msimbazi Simba ambapo katika mchezo wake wakwanza tuu dhidi ya Prisons alifunga bao tatu akiwa na uzi wa Msimbazi.

Saidoo Ntibazonkiza akishangilia pamoja na Clatous Chama.

Kiungo huyo raia wa Burundi alianza vyema akiwa na Geita Gold akihusika katika mabao ya timu hiyo kwa kutoa pasi za mabao ama kufunga mwenyewe na pia alipohamia Simba aliendelea na moto wake wakufunga na kutoa pasi za mabao na kumfanya kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Simba chini ya kocha Robertinho.

Mpaka sasa ikiwa imebaki michezo miwili Saido mwenye miaka 36 ndie mchezaji aliyehusika katika mabao mengi zaidi katika Ligi Kuu ya NBC, akiwa amefunga mabao 10 na kutoa pasi 12 za mabao.

Ni kweli katika Ligi kuna viungo wengi wengine wazuri na bora kama kina Aziz Ki, Clatous Chama, James Akamiko, Feisal Salum na Sixtus Sabilo lakino wote hao hawamfikii Saidoo kwa namba katika takwimu zao.

Saidoo Ntibazonkiza (katikati) akiwaacha wachezaji wa Yanga katika Kariakoo Derby.

Ikiwa imebaki michezo miwili kwa Ligi kumalizika ni wazi huenda Saido akamaliza akiwa ndie mchezaji aliyehusika katika mabao mengi zaidi hivyo pasi na shaka anastahili kuwa kiungo bora wa msimu lakini pia akawepo katika kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa kigeni.

Babu Saidoo anazeeka na utamu wake na msimu huu amepatia tena sio katika nadharia ni namba ndio zinaongea ni vyema sasa apewe maua yake.

 

Sambaza....