Blog

Stars yatua Algiers kuwakabili El Khadra

Sambaza....

Timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars, imetua Algiers, Algeria na kupokelewa na balozi wa Tanzania nchini humo mheshimiwa Omar Yusuf Mzee.

Stars inayolewa na kocha Salum Mayanga akisaidiwa na Ally Bushir, ipo nchini humo kwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaochezwa kwenye tarehe za kalenda ya FIFA Machi 22, 2018.

Itakumbukwa mara ya mwisho Stars kucheza nchini humo, ilikuwa ni Novemba 18, 2015 ambapo Stars ilikubali kichapo cha mabao 7-0 huo ulikuwa ni mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia nchini Urusi.

Awamu hii Stars inakutana tena na “El Khadra” (The Green) katika mchezo huo wa kirafiki, huku Stars ikionekana kuwa mabadiliko makubwa kunako benchi lake la ufundi na baadhi ya wachezaji.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x