Aidha Feisal pia amesema hawezi tena kurudi Yanga kwani hana uhuru tena na hafurahii kufanya kazi na Wananchi hivyo ni vyema akaruhusiwa kuondoka zake akacheze sehemu nyingine.
Rais huyo wa Yanga pia hakua na shida na Feisal na kusema wamempa machaguo ambayo yeye mwenyewe ataamua alifuate lipi ili aweze kuendelea kucheza soka.
Ni kweli katika Ligi kuna viungo wengi wengine wazuri na bora kama kina Aziz Ki, Clatous Chama, James Akamiko, Feisal Salum na Sixtus Sabilo lakino wote hao hawamfikii Saidoo
Mwisho wa siku ni Mchezaji wa timu ya Taifa huwezi kumuacha kwa sababu hachezi , hata mimi nimecheza timu ya Taifa wakati nilikuwa sichezi timu ya Klabu,
Adel Amrouche aliyetangazwa hivi karibuni kupewa mikoba ya Stars amewajumuisha wachezaji wengi wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi akichanganya na baadhi wanaocheza Ligi ya ndani.