Mataifa 12 yenye rank (viwango) vya juu kwa muda wa miaka mitano (Caf 5 year Ranking) yanapata nafasi ya kuingiza timu 2 katika kila mashindano ya vilabu barani Africa na kufanya nchi kuwa na wawakilishi wanne kila mwaka.
Mwaka huu Caf wametumia hicho kigezo pia kwa kuangalia Club perfomance ranking (kiwango cha timu shiriki za nchi husika katika mashindano ya vilabu Afrika) vya miaka mitano kuanzia 2012 mpaka 2016 ndio maana msimu huu utaona Zambia nao wakifaidika na hilo kwa sababu Zesco miaka hii ya karibuni imepatia sana points (alama ambazo zimeinufaisha nchi kwa ujumla kwa kutoa wawakilishi wengi kwenye michuano hii ya vilabu barani Afrika).
Unazipataje hizo points (alama?). Ni hivi kila Taifa hupata points(alama) kulingana na perfomance (maendeleo) ya timu zake katika mashindano ya vilabu kama ifuatavyo.
Ukiwa bingwa mashindano ya klabu bingwa nchi inapata points (alama) 5 na ukiwa bingwa Confederation cup (kombe la shirikisho barani Afrika) nchi inapata points (alama) 4.
Ukiwa finalist (kufika fainali ) ya klabu bingwa nchi inapata points (alama) 4 wakati hatua hiyo confederation cup(kombe la shirikisho barani Afrika) nchi inapata points(alama) 3.
Ukiishia hatua ya nusu fainali klabu bingwa nchi inapata points (alama) 3 na confederation cup nchi inapata points (alama) 2.
Klabu ikishika nafasi ya tatu hatua ya makundi klabu bingwa nchi inapata points ( alama) 2 na hatua hiyo hiyo kwenye confederation cup ( kombe la shirikisho barani Afrika) nchi inapata point (alama)1.
Ukiingia hatua ya makundi klabu bingwa nchi inapata point moja na hatua hiyo hiyo confederation cup(kombe la shirikisho barani Afrika) nchi inapata point(alama) moja.
Kwa msimu huu kulingana na caf 5 year ranking ya kuanzia mwaka 2012-2016 Nchi zilizokua na points (alama) ni kama ifuatavyo:
1)Egypty 85
2)Tunisia 76
3)DRC 70
4)Algeria 62
5)South Africa 45
6)Morroco 41
7)Sudan 35
8)Ivory Cost 21
9)Zambia 18
10)Congo 16
11)Mali 15
12)Nigeria 13
13)Cameroon 12
14)Libya 8
15)Ghana 7
16)Tanzania 5
17)Angola 3
18)Ethiopia 2
Na hapo hizo 12 za juu ndizo zimetoa wawakilishi wawili kila michuano ya vilabu barani Africa msimu huu, Tuiombee Yanga ifike mbali ili tupate points(alama) ili ndani ya five years caf ranking ijayo Taifa lipate wawakilishi wawili Ukiangalia kwa makini hili sio suala dogo ni suala la kimkakati kwa nchi kama nchi na vilabu husika.
Ndipo hapa vilabu vinatakiwa viwe pamoja kwenye michuano hii ya kimataifa ili vilabu vingi vinufaike.
Nchi iweze kutoa wawakilishi wanne na siyo wawili kama ilivyo kwa sasa.