Yanga mazoezini
Shirikisho Afrika

Ten- mmoja tu ataukosa mchezo dhidi ya Rayon

Sambaza....

Kikosi cha Yanga SC, kesho kitashuka kunako uwanja wa taifa kuvaana na Rayon Sports ya Rwanda katika mchezo wa hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika

Kuelekea katika mchezo huo, Yanga itakosa huduma ya kiungo wake Said Juma “Makapu” akitumika adhabu ya kuwa na kadi mbili za njano ambapo kwa mujibu wa kanuni, mchezaji anapaswa kukosa mchezo mmoja endapo akifikisha idadi ya kadi hizo

Akiongea na mwandishi wa tovuti hii Afsa Habari wa klabu hiyo, Dismas Ten alithibitisha kukosa huduma ya mchezaji huyo kutokana na adhabu hiyo

“Kila kitu kinakwenda sawa timu ipo Dar es salaam tunasubiri mchezo Jumatano, wachezaji wana hali nzuri, mchezaji ambaye atakosekana ni Saidi Juma kutokana na kuwa na kadi mbili za njano lakini wachezaji wote wapo na wana hali nzuri”

Aidha Ten, alisema kuwa kile kitachotekea uwanjani ni sehemu ya maandalizi ambayo wameyafanya kwa kuwa wamejiandaa kushinda katika mchezo huo

“Mwisho wa siku kile ambacho kitatokea uwanjani ni sehemu maandalizi ya mchezo, kwa sababu tulihakikisha tunajiandaa vizuri ili tuweze kushinda mchezo ” alisema Ten

Yanga itamkosa kiungo huyo, huku ikitakiwa kushinda katika mchezo huo ili kujijengea mazingira mazuri ya kuendelea kusalia kunako michuano hiyo ya pili kwa ukubwa, barani Afrika kwa ngazi ya vilabu

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x