Blog

Tenga ateuliwa kuongoza BMT

Sambaza....

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo Dk. Harrison Mwakyembe amemteua raisi wa zamani wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Leodigar Chilla Tenga kuwa mwenyekiti wa Baraza la michezo nchini (BMT).

Katika taarifa hiyo iliyotolewa leo na kaimu mkuu wa idara ya mawasiliano serikalini, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo Lorietha Laurence imesema kuwa Mwakyembe ameteuwa wajumbe tisa kuongoza Baraza hilo.

Katika uteuzi huo yupo Yusuf Singo mkurugenzi wa maendeleo ya michezo, Dk Edcome Shirimam Kamishina Wizara ya Elimu, sayansi teknorojia na mafunzo ya ufundi na Mohammed Kiganja akiendelea kuwa katibu wa Baraza hilo.

Pia kuna wajumbe sita ambao ni Beatrice Singano, kanali mstaafu Juma Ikangaa, Profesa Mkumbwa Mtambo, Rehema Seif Madenge, Salmin Kaniki pia mwansheria Damas Ndumbaro ameingia kwenye uteuzi huo.

Uteuzi huo umefuatia baada waziri Mwakyembe kuuvunja uongozi wa awali wa Baraza hilo uliokuwa chini ya mwenyekiti Dioniz Malinzi mwezi Julai mwaka jana, na kuipa madaraka sekretarieti chini ya Mohammed Kiganja hadi utakapoteuliwa uongozi mpya.

 

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x