Mabingwa Afrika

This is Simba!

Sambaza....

 1. Mlidhani tungefeli, dimbani mkafurika, Kule Iringa Lipuli, ulimi ukawatoka, Simba robo fainali, tumetinga tunawaka, THIS IS SIMBA mkubali, TAIFA KUBWA Afrika!

 

 1. ZIMBWE kawatakabali, dogo pilikapilika, Katokea nyuma mbali, kawapeleka peleka, Kuchanya sio kutali, kati refa kanyooka, THIS IS SIMBA mkubali, TAIFA KUBWA Afrika!

 

 1. NIYONZIMA ni mkali, kweli FAZA sio kaka, NIYO kama ZIRAILI, VITA wameadhirika, BAMUTU BA KONGO chali, bamesuka na kusuka, THIS IS SIMBA mkubali, TAIFA KUBWA Afrika!

 

 1. MZAMIRU yule kweli, wa kuuzwa hata BAKA, Kapiga VIBASKELI, VITA wakaweweseka, Mzamiru BARADHULI, ASENO wanamtaka, THIS IS SIMBA mkubali, TAIFA KUBWA Afrika!

 

 1. WAWA kidume RIJALI, MCHECHE FULU KUWAKA, KANGI LUGOLA mithili, mfukoni kawaweka, Wawa Sege PASIKALI, kumpita ni mashaka, THIS IS SIMBA mkubali, TAIFA KUBWA Afrika!

 

 1. Ingekuwa ni kusali, NYONI Paroko hakika, Nyoni kakaa na mali, majeruhi ametoka, Lakini ni afadhali, kapona kaimarika, THIS IS SIMBA mkubali, TAIFA KUBWA Afrika!

 

 1. MWAMBA CHAMA ni asali, mtamu kanyumbulika, Kagawa ZA MAJI BILI, maji safi MAJI TAKA, CHOTA CHAMA jama dili, kambani kamba kaweka, THIS IS SIMBA mkubali, TAIFA KUBWA Afrika!

 

 1. Mkubwa BOCCO-MAGOLI, kiwango hakijashuka, Japo hakuwakong’oli, kuwachosha kahusika, Magoli yale mawili, yametutosha kuvuka, THIS IS SIMBA mkubali, TAIFA KUBWA Afrika!

 

 1. Huyo ZANA KULIBALI, kaambaa kama nyoka, Ni kama BEKAMU nguli, MAJALO zamiminika, Kakomaa kama KULI, YANGA WANAMKUMBUKA!, THIS IS SIMBA mkubali, TAIFA KUBWA Afrika!

 

 1. Hii Simba SAMPULI, BAKA YA ILE MIAKA, YATULIZA BOLI TULI, MPIRA KWENYE UKOKA, YANGA KUCHA HAWALALI, KWANINI WANATESEKA?, THIS IS SIMBA mkubali, TAIFA KUBWA Afrika!

 

 1. PUNGENI TU MADOGOLI, Sisi mbele twanyooka, Simba ni KISULISULI, Afrika tunasifika, YANGA FUNGENI BAKULI!, Simba hii FYEKAFYEKA!, THIS IS SIMBA mkubali, TAIFA KUBWA Afrika!

 

KUTOKA: Mkini na Alpha WAHENGA WA TAMBAZA (0766841987 na 0655595900) DODOMA-TANZANIA

HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.