Sambaza....

Mtanzania Simon HappyGod Msuva ameshindwa kuifikia ndoto yake ya kucheza hatua ya robo fainali ya Michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya timu yake ya Difaa El Jadidi kutoka sare ya bao 1-1 na TP Mazembe katika mchezo wa mwisho wa B na kushika nafasi ya tatu.

Katika mchezo Simon Msuva amecheza dakika zote 90 ambapo timu yake walikuwa wakiomba ES Setif kupoteza mchezo wao dhidi ya MC Alger huku wao wakitakiwa kuwafunga TP Mazembe ili kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua ya Robo fainali.

TP Mazembe ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Ben Malango Ngita kwa njia ya penati katika dakika ya 87 kabla ya Hussein Khokhouche kusawazisha katika dakika ya 90 kuwahakikishia sare Difaa El Jadidi.

Matokeo hayo yanawafanya Difaa El Jadidi kufikisha alama 6 nyuma ya vinara wawili ES Setif wenye alama 8 na TP Mazembe wenye alama 12 wakati MC Alger wakishika mkia wakiwa na alama 5.

Sambaza....