Sambaza....

Kwa kuutazamia mchezo kati wenyeji Simba sc dhidi ya Azam fc, kwa hakika utakuwa ni mchezo mzuri na wenye ushindani mkubwa kwa kuzingatia ubora mabenchi ya ufundi na nafasi katika msimamo wa ligi ikiongeaza changamoto kwenye mchezo huo

Simba sc, ambao ni vinara wa ligi hiyo mpaka sasa wakiwa na alama 38 baada ya kushuka dimba mara 16, bila shaka wataingia katika mchezo huo kwa lengo moja la kusaka alama tatu ili kuendelea kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuwania ubingwa

Kiufundi

Simba sc, waliochini ya kocha Pierre Lechantre wanaonekana kubadilisha mfumo wao wa uchezaji kutoka kwenye 3-5-2 na kurudi kwenye 4-4-2 au 4-3-3 huku wakiimalika zaidi kwenye aina yao ya uchezaji

Simba ni wazuri kwenye pressing na cut off, ina viungo wazuri kwenye pass skills ya pressing game, high speed pass na pass combination yao iko vizuri

Taarifa

Tarehe Muda Ligi Msimu Mwisho
07/02/2018 4:00 pm TPL 2017-2018 90'

Ubora wa Simba sc unaanzia katikati ya kiwanja watu kama Jonas Mkude, Said Ndemla na Mzamir Yasin kwa pamoja hawa ndio mzizi wa timu kwenye offensive patterns na defensive patterns

Jonas Mkude usimama kama kiungo wa ulinzi huyu ubeba majukumu yote ya timu kwenye kujilinda ili kuhakikisha anailinda vema ile back line huku akiisaidia timu kujenga mashambulizi, ni mzuri kwenye blocking, kupora mipira huku akitoa backup kubwa kwa Said Ndemla, ili kuwatawanya viungo pinzani na kumfanya Ndemla kuwa huru kuchezesha timu ambaye katika mchezo uliopita alioneka kucheza kama box to box midfield huku Mzamir Yasin akitumika free role task kukamilisha kiungo wa pili wa kuchezesha timu kwenye mfumo wa 4-3-3

Safu ya ushambuliaji yao inaonekana kuimalika vena Emmanuel Okwi ambaye ucheza kama mshambuliaji wa pili (Auxiliary attacker) amekuwa akipokea muunganiko mzuri wa kimbinu kutoka kwa viungo wa kati, huku akiisaidia timu kujenga angle ya mashambulizi. John Bocco huyu ni target man na kwa hakika katika michezo miwili iliyopita amaeonekana kurejesha makali yake kwa kufunga mabao mengi hali inayomfanya kuingia katika mchezo huu akiwa vizuri kisaikolojia, Shiza Kichuya bado ataendelea kutumika kama Orthodox left footer akitokea upande wa kulia kwa kufanya technical dribbling au switching to unlock kuindoa safu ya ulinzi ya Azam ikiwa kwenye mstari

 

Safu yao ya ulinzi bila shaka itaongozwa na Juuko Murshid na Erasto Nyoni hawa wameonekana kucheza kwa uelewano mkubwa kama mabeki wa kati, huku Shomari Kapombe na Asante Kwasi wakisimama kama walinzi wapembeni nao wamekuwa msaada mkubwa pale timu inapojenga mashambulizi yao kutokea chini

Kuna wa kati hufanya makosa ya kuchelewa kujipanga na kushindwa kufanya pre marking, hivyo katika mchezo huu wanapaswa kuongeza umakini kwa maana wanakutana na timu ambayo ipo very tactical na wachezaji wenye uwezo wa kutumia makosa yao

Nb Simba kwa sasa wanaonekana kuimalika vema kwenye tactical philosophy, tactical focus, team technical understanding, attacking tactics na finishing a speed pia wana confidence

Azam fc, wapo katika nafasi ya tatu wakiwa na alama zao 33, ni wazi wataingia katika mchezo huu kwa lengo la kutaka alama tatu muhimu ili kuendelea kujiweka katika mazingira mazuri ya kuwania taji

PosTimuPWDLFAGDPts
1Simba SC2151494719423125298494
2Yanga SC2071424322343122221469
3Azam FC2111195339320153167410
4Kagera Sugar FC210617178175217-42254
5Tanzania Prisons208597673177201-24253

Kiufundi pia Azam fc wapo vizuri na mara nyingi wamekuwa wakitumia mfumo wa 4-4-2 ni wazuri kwenye pressing na wana viungo wazuri wanaojua majukumu yao uwanjani

Kocha Aristica Cioba amekuwa akipenda sana kutumia viungo wawili asilia katikati ya kiwanja, lakini bila shaka katika mchezo huu anaweza kufanya mabadiliko kidogo kwenye eneo hili kwa kuongeza kiungo mmoja wa ukabaji ili kuwazibiti Simba katikati ya kiwanja

Stephen Kingue amekuwa akicheza kama kiungo wa ukabaji, huku Salum Abubakar akisimama kama kiungo wa juu ambapo wamekuwa na uelewano mzuri kutokea kati na mara nyingi hupenda kujenga box kwenye eneo la kiungo huku msingi mkuu wa timu kwenye kujilinda na kushambulia ukiwa pembeni

Enock Atta na Joseph Mahundi hawa hutumika kama sprinter kutokana kasi yao husaidia sana kukimbiza mipira na kumchosha mpinzani pembeni mwa kiwanja

Safu yao ya ushambuliaji pia inaonekana sio mbaya ni wazuri sana kwenye kucheza klosi, wamekuwa wakifunga mabao kutokea pembeni watu kama Yahaya Zayed na Shaban Iddi ni wazuri kwenye kujipanga na kumalizia kazi zilizofanywa na viungo wao

Safu yao ya ulinzi bila shaka itakuwa chini ya Agrey Morris na Yakub Mohammend kama walinzi wa kati huku Bruce Kangwa na Himid Mao wakicheza kama walinzi wa pembeni wamekuwa wakicheza kwa uelewano mkubwa huku wakijitahidi kuficha makosa lakini huu ni mchezo watakaohitaji msaada mkubwa kutoka kwa viungo wao wa kati ili kuua muunganiko wa kimbinu wa washambuliaji na viungo wa Simba

Azam fc wanamakosa ya kuruhusu sana kushambuliwa na kushindwa kufanya marking sawasawa hivyo katika mchezo huu watatakiwa kuwa makini sana, kwa maana inakutana mpinzani kwenye wachezaji wengi wenye uwezo wa kuamua mchezo second balls ama counter attacking zinaweza zikawaumiza Said Ndemla, Mzamir Yasin na Emmanuel Okwi wanapaswa kuwachunga sana

Pia Azam fc, wameimalika sana kwenye tactical philosophy, tactical focus, team technical understanding na pressing tactics ni wazuri kwenye kumiliki mpira japo katika mchezo huu long ball game na counter attacking tactics inaweza kuwa msaada mkubwa kwao

Nb Aristica Cioba anapaswa kuwa makini sana na aina ya uchezaji wa Simba hasa kwenye eneo la kiungo, anaweza kuwa ni viungo wawili wa ukabaji (double pivot) pia mfumo akatumia 4-2-3-1 hii ni flexible formation ni rahisi sana kwenda kwenye mfumo mwingine

Pia kila timu itapaswa kuongeza umakini kwenye timing of overlapping kutokana na pende zote kuwa na watu wenye kasi na uwezo wa kuamua matokeo

Sambaza....