Sambaza....

Sekretarieti ya shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF imewapeleka kwenye kamati ya maadili viongozi wanne kwa kughuhushi na udanganyifu

Viongozi walioshtakiwa kwenye ya Kamati ya maadili ni msimamizi wa kituo cha Mtwara Dunstan Mkundi, Katibu wa Chama cha soka mkoa wa Mtwara Kizito Mbano, muhasibu msaidizi wa klabu ya Simba Suleiman Kahumbu na Katibu msaidizi wa klabu ya Ndanda FC ya Mtwara Seleman Kachele

Sekretariati inawashitaki viongozi hao kwa makosa ya kughushi pamoja na udanganyifu wa mapato kwenye mchezo namba 94 kati ya Ndanda FC ya Mtwara dhidi ya Simba ya Dar es salaam uliochezwa disemba 30, 2017 kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara

Mchezo ambao ulimalizika kwa Simba kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda FC

Kwa tuhuma hizo viongozi hao watatakiwa kufikia mbele ya kamati januari 18, 2018

Kamati ya maadili iko chini ya mwenyekiti wakili Hamidu Mwezeleni, makamu mwenyekiti Wakili Steven Zangira, wajumbe Grorious Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhresa

Sambaza....