Sambaza....

MARA ya mwisho Yanga SC kushinda katika ‘Dar es Salaam-Pacha’ ilikuwa Machi 2016 waliposhinda 2-0, baada ya hapo, mabingwa hao mara 27 wa kihistoria wa ligi kuu Tanzania Bara wamepoteza mara mbili na kutoa sare michezo miwili katika game nne za ligi zilizopita. Kiujumla, katika michuano yote Yanga haijashinda dhdi ya mahasimu wao Simba SC katika michezo sita mfululizo il;iyopita.

LEO…..

‘Timu ya Wananchi’ kama navyopenda kuiita inaingia uwanjani katika ‘PACHA’ ya kwanza msimu huu-mchezo wa tano tu wa msimu huku wakiwa na alama 12 ( pointi mbili mbele ya Simba ambao katika michezo yao mitano wameshapoteza mara moja na sare moja-Ndanda FC 0-0 Simba, Mbao FC 1-0 Simba)

KIUCHEZAJI…..

Kocha wa Yanga, Mcongo, Zahera Mwinyi atawaksa kiungo Juma Mahadhi na mlinzi wa kulia Juma Abdul. Soka la kushambulia katika michezo minne iliyopita limeifanya kikosi chake kutikisa nyavu mara tisa katka michezo minne iliyopita; washambuliaji wake Mcongo, Heritier Makambo na Mrundi, Amis Tambwe wakifunga mara mbili kila mmoja.

Dalili zimeonyesha dhahiri kwamba, Yanga wameanza msimu kwa stahili ya aina ake-ushinsi asilimia 100 na watapaswa kuilazimisha pia Simba kurudi nyuma ili kupata matokeo, lakini habari inaweza kuwa tofauti kama safu yao ya ulinzi itaendelea kuonyesha kasoro kubwa kama katika michezo dhidi ya Mtibwa Sugar FC na Stand United ambayo waliruhusu jumla ya magoli mawili.

Ili kutimiza ndoto-kushinda kwa mara ya kwanza baada ya michezo minne ya ligi dhidi ya mahasimu. Katika mchezo dhidi ya Stand United, licha ya kufunga moja ya magoli manne ya timu yake mlinzi wa kati, Vicent Andrew alikuwa dhaifu wakati Mrundi, Alex Kitenge alipofunga ‘Hat Trick; katika game hiyo iliyomalizika 4-3.

Andrew ameonekana kurudi na katika michezo miwili dhidi ya Coastal Union na Singida United wiki iliyopita aliiongoza safu yake ya ulinzi kumaliza dakika 180 pasipo kuruhusu goli. Hii inaweza kupunguza hofu kubwa iliyopo katika safu ya ulinzi hasa ile ya kati kuelekea mchezo ambao, hapana shaka, kocha wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussems atawaanzisha washambuliaji wake wa kimataifa, Mnyarwanda, Meddie Kagere na Mganda, Emmanuel Okwi.

Licha ya Ibrahim Ajib kuonekana ni tishio zaidi kwa wapnzani , Mrisho Ngassa na Deus Kaseke kutokana na uwezo wao wa kumiliki mpira na kupiga pasi, huku uwezo wa Makamb na ‘kufufuka’ kwa Tambwe kukizidi kuipa mguvu zaidi Yanga na kuonekana tishio katika mashambulizi, Zahera anaweza kujikuta katika wakati mgumu kama kijana Paul Godfrey atapoteza kujiamini.

Mchezaji huyo namba mbili aliyepandishwa jkikosi cha kwanza anastahili kuanza mchezo wa leo kutokana na kucheza vizuri katika michezo iliyopita baada ya Juma kukosekana kutokana na majeraha. Yanga hucheza vizuri na kwa maelewano kwa dakika 60-75, lakini baada ya hapo hadithi huwa tofauti kabisa huku ‘watuhumiwa’ wa kwanza katika hilo wakiwa viungo wa kati.

Mcongo, Papy Tshishimbi na Feisal Salum ‘Fei Toto’ wameonekana kuwa na matatizo makubwa na mara kadhaa kumfanya Kaseke kuondoka katika nafasi yake na kusogea zaidi kati. Viungo hao walinzi wanapaswa kuboresha uwezo wao wa kupiga pasi zinazofika, umakini na upotezaji wa mpira mara kwa mara, huku Fei Toto akitakiwa zaidi kutazama uchezaji wake wa faulo za karibu na eneo lake la hatari kwa sababu Simba wanae-Okwi mmoja wa wapigaji mahiri wa mipira iliyokufa.

Kukosa nguvvu kwa safu ya kiungo ya Yanga katika michezo minne iliyopita- hasa udhaifu wa kucheza pasi zinazofika kutaiponza. Said Juma Makapu na Mzimbabwe, Thaban Kamusoko wanahitajika lakini tayari kocha Zahera ana kikosi chake cha kwanza na si rahisi kuwaacha nje, Fei Toto na Tshishimbi.

Katika mchezo ambao Yanga ilionyesha kiwango cha chini katika ulinzi dhidi ya Stand United safu hiyo ya kiungo ilionekana kutokuwa na msaada na mchango wao wa kulinda unatia shaka mno .Kitendo cha kocha Zahera kushindwa kumpa nafasi yeyote katika Kamusoko au Makapu kuanza mchezo kunaweza kuwaponza zaidi Yanga katika mchezo wa leo kwa sababu wachezaji hao wawili ni wakabaji ambao wanacheza pia vizuri faulo zisizoonekana na waamuzi.

Zahera anaweza kumuanzisha Makapu mahala pa Fei Toto ama Kamusoko ili kucheza na viungo wake wane-Ajib, Ngassa, Kaseke na Tshishimbi kama kweli anahitaji kumaliza ndoto za kutoifunga Simba kwa misimu miwili na zaidi sasa.

Sawa, Yanga imeonekana ina uwezo mkubwa wa kumiliki mira, lakini mambo yanaweza kuwa tofauti leo kama hawatosahihisha haraka matatizo yao katika eneo la kiungo na umakini katika safu ya ulinzi wa kati. Wanaweza kufunga goli/magoli katika mchezo wa leo lakini wasiwasi mkubwa ni jinsi timu hiyo inavyojilinda kuanzia kati mwa uwanja.

MFUMO…..

4-5-1 ningemshauri Zahera kuanza mchezo na mfumo huu, kwanza ni mzuri katika ulinzi na naifanya timu kupeeka mashambulizi timilifu yaliyopangiliwa. Anao wachezaji wazuri ambao wanaweza kumsaidia kupata ushindi; Gofrey, Gadiel Michael, nahodha Kelvin Yondan na Vicent Andrew wanaweza kuanza kama walinzi wanne baada ya golikipa Beno Kakolanya.

Kamusoko/Makapu/Fiisal, Tshishimbi, Kaseke, Ngassa na Ajib wanaweza kuanza kama watu watano katika kiungo ambao watakuwa na juukumu la kuzuia, kuandaa mashambulizi na kumchezesha mshambulizi pekee Makambo/Tambwe.

Samba wanaonekana watatumia mdfumo wa 4-3-3 na kama itakuwa hivyo inamaanisha ni rahisi kwao kuwaanzisha Shomari Kapombe, Mohamed Hussein ‘Zimbwe JR’, Erasto Nyoni na Paschal Wawa katika ngome, James Kotei, Jonas Mkude na Mzambia, Chama katika kiungo na Shiza Kichuya, Kagere na Okwi katika mashambulizi ili kuwabana na kuwanyima uhuru wa kuchezea mpira Yanga wanatakiwa kuwa wengi kati ya uwanja na kucheza mchezo wa moja kwa moja wanaposhambulia.

MSHINDI YANGA…

Kete yangu naiweka Yanga kwa sababu wanaingia katika mchezo huu bila presha kubwa kutokana na aina ya vikosi vya timu zote mbili vilivyotengenezwa. Samba wanathamani kubwa ya usajili lakini ndani ya uwanja katika michezo mitano iliyopita wameonekana kushindwa kucheza kitimu.

Hii ni mechi ya kwanza kwa makocha Zahera na Aussems lakini bado wanaweza kutumia uzoefu wao kiufundishaji kupunguza presha ya mashabiki wao na katika ili Aessems anaweza kuwa mhanga wa kwanza. Aliona kilichomkuta, Mwanza wakati timu yake ikiwa nyuma na dakika zikiyoyoma dhidi ya Mbao FC.

Kutopata ushindi kwa Simba katika mchezo huu kutaanza kumuweka njia panda Aessems na kama watapoteza mchezo mwingine wowote anaweza kuanza kukalia ‘kuti kati’- ni dhahiri kikosi chake hakichezi vizuri katika michezo mitano iliyopita na kuelekea mchezo wake wa kwanza wa Pacha ya Dar es Salaam kocha huyo raia wa Ubelgiji anapaswa kurekebisha mambo kadhaa.

Simba wanaonekana pia hawana pumzi ya kutosha kama iliyo kwa Yanga na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja tu ndiyo umekuwa ukiwasaidia zaidi kupata matokeo. Hawatengenezi nafasi nyingi za kufunga, nao pia wana tatizo la safu yao ya kiungo kupoteza mipira hovyo katikati ya uwanja.

Kutokana na hili, wakitanguliwa tu kufungwa basi mchezo utakuwa mgumu mno kwao, na bila shaka watapoteza mchezo huu kutokana na kwamba wanakwenda kucheza na wapinzani ambao hawana presha kubwa kuliko wao.

Sambaza....