Ligi Kuu

Yanga SC yajipanga dhidi ya Ruvu shooting

Sambaza....

Mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga sc, wapo kwenye maandalizi kabambe ya kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika dhidi ya Ruvu shooting ya Pwani

Katika mchezo huo wa ligi kuu utakaofanyika Jumapili kunako dimba la Uhuru jijini Dar es salaam, huenda Yanga ikaendelea kuwakosa mshambuliaji Donald Ngoma na mlinzi Abdallah Shaibu “Ninja” waliomajeruhi

Akiongoea na mwandishi wa kandanda, Ten alisema maandalizi yao kuelekea kwenye mchezo huo yapo vizuri na kikosi kiliendelea na mazoezi yake hii leo

“Timu imeendelea na mazoezi kama kawaida leo imefanya pia na kesho itaendelea na program za mwalimu”

Katika hatua nyingine Ten alizungumzia kuhusu mlinzi wao Festo Kayembe raia wa Kongo, kuwa ITC yake bado haijapatikana na hayupo nchini kwa sasa

Pia Ten alihabarisha kibali cha kufanyia kazi cha kocha mkuu George Lwandamina kimepatikana na anaendelea na majukumu yake kama kawaida.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x