Sambaza....

Yanga sc itakumbana na Majimaji FC katika hatua ya 16 bora, ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC)

Katika droo iliyofanyika leo kunako kituo cha Azam TV, michezo yote ya hatua hiyo ya michuano ya kombe la shirikisho la soka nchini (TFF) imepangwa kufanyika Februari 22 na 25

Pia ratiba hiyo inaonesha kuwa Azam FC itavaana na timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) ya jijini Dar es salaam, huku JKT Tanzania wataikaribisha Ndanda FC kunako uwanja wa Mbweni jijini Dar es salaam

Tanzania Prisons watakuwa wageni wa Kiluvya United kunako dimba la Filbert Bayi, Kibaha pwani, Singida United na Polisi Tanzania mchezo utakaofanyika kwenye uwanja wa Namfua

Mji Njombe watakipiga na Mbao FC kunako dimba la sabasaba mjini Njombe, katika hatua hii mkoani Shinyanga itapigwa michezo miwili ambapo Stand United “Chama la wana” dhidi ya Dodomo FC huku Buseresere wakiwakaribisha mabingwa wa zamani wa ligi kuu Mtibwa Sugar kunako uwanja wa Kahama

Na katika mchezo ambao unaweza kuvuta hisia za mashabiki wengi wa soka nchini, ni Majimaji FC dhidi ya Yanga sc hii ni kutokana na historia ya vilabu hivi ya michezo inayofanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea

Sambaza....