Sambaza....

Unakumbuka kipindi kile unakua kua hadi unaanza shule ya ‘VIdudu’ kule kijijini kwenu?..

Unakumbuka tukio gani la enzi hizo?? Au basi, unakumbuka uliwahi kuambiwa kauli hii,
“Ukienda kule Brazil, hata ukimkuta muuza mkaa ujue ni fundi wa boli.”

Basi bwana hao ‘wauza mkaa’ ni akina Ronaldinho, Neymar, Marcelo na mafundi wengine wa Kibrazil ambao walitokea kuliteka soka la Ulaya na duniani kwa ujumla.

Ronaldinho Gaucho.

Ukiachana na kina Dinho ambaye amefanya watu wengi wa kizazi hiki waupende mpira wa miguu, ukiachanya na jamaa huyo anayecheka muda wote kuna jina la Marcelo.

Hakuna mpira wa hewani uliomshinda huyu jamaa, chenga zake, kanzu kwa wenzake na zaidi vituko vyake awapo uwanjani ni rahisi kumtambua.

Ameaga nyumbani kwake pale Santiago Bernabeu baada ya kuishi pale kwa miaka 16 na sasa anaenda zake kuishi nchi ya mbali.

Marcello na Ronaldo.

Unakumbuka urafiki wake na Cristiano Ronaldo?.. Vipi ukaribu wake na akina Toni Kroos na Luka Modric ‘Mtu mfupi?.’

Anyway, Ndio hivyo tena, Marcelo amemaliza kila kitu akiwa na Real Madrid na bahati iliyoje kwake katika msimu wake wa mwisho alipewa kitambaa cha unahodha na amenyanyua La Liga na UCL.

Pamoja na kucheza nafasi ya ulinzi wa kushoto, Marcelo alikuwa mhimili mkubwa wa kushambulia kwa upande wake na amefunga ‘mabao ya kideoni’ kutokana na kasi na ufundi wake.

Marcello akipiga shuti langoni mwa Athletico Madrid na kufunga katika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Kuna ambaye amesahau bao lake kwenye fainali ya UCL 2014 dhidi ya Atletico Madrid nimtumie clip? .

Basi, kuna aliyesahau control za viwango za mipira ya juu kwa ‘Muuza mkaa’ huyu kutoka nchi yenye Uwanja wa Maraccana? 🇧🇷.

By the Way tangu Madrid iumbwe hakuna mchezaji aliyewahi kubeba mataji mengi kama ‘Muuza Mkaa’ huyu. Sasa anaondoka na kumbukumbu ya kubeba makombe 15 akiwa na Madrid.

NB: Huyu ndio yule muuza mkaa kutoka nchi ya akina Fraga na Jaja!

Sambaza....