KYLIAN MBAPPÉ(25) ni miongoni mwa wachezaji bora sana kwa sasa ambao wanatabiriwa makubwa Duniani, tayari ameanza kutokea kwenye nominations ya Tuzo kubwa za mpira wa miguu akiwa na umri mdogo.
Mbappe pia huenda hivi karibuni akaanza kuchukua moja baada ya nyingine kama akibaki na kuendeleza ubora na daraja alilonalo kwa sasa.
Real Madrid kupata nafasi ya kumsajili na kumiliki mchezaji wa aina hii katika nyakati hizi ambazo ana ubora wa juu na umri wake ni mdogo basi hapa wamecheza karata nzuri sana, tazama wale kina Rodrygo, Valverde, Vinicius JR, Jude Bellingham, Arder Güler na wengineo namna ambavyo wanafanya vizuri kwa sasa na wakati ambao wamefika, it’s just the Best Timing.
Rais wa Klabu Mzee Fiorentino Perez kuna sehemu nyingi sana katika uongozi wake amefanikiwa kwa kiasi kikubwa, kwanza namna ambavyo ameondoa taratibu yale majina makubwa ya wachezaji ambao tayari walikuwa wamepata mafanikio ndani ya Klabu na hata waliobaki ameona hawana muda mrefu pale kabla ya miaka miwili ameleta vijana ambao tayari wameanza kuibeba Timu kwenye mashindano makubwa.
Pili, kuna eneo kubwa sana la matumizi ya pesa kwa Misimu hii Mitatu amefanikiwa kwa hawa wachezaji namna ambavyo ametumia pesa kusajili, ukiangalia kiwango cha mchezaji husika wakati huo na pesa aliyotoa basi utaona amefanikiwa sana kucheza na hizi dili! Mwisho, tazama vipaji vya hao wachezaji aliowaleta moja kwa moja pale ndio utaona kuna kazi kubwa ya Scouting Team ambayo imefanywa mpaka wamepata majina ya wachezaji wazuri ambao amekubali kuwapa mikataba.
Simply! Kuna mstari mdogo sana wa mchezaji kufeli au kutokuwa na kipaji kwa sasa kucheza ndani ya Santiago Bernabeu, maeneo mengi sana wamefanikiwa na ndani ya hii Miaka Kumi unaona wana Timu nzuri ambayo itatumika kwenye soka la ushindani na wakapata uhakika wa kushinda makombe ndani ya Klabu kubwa kama Real Madrid, Carlo Ancelotti pia kitu kizuri anajua kuwatumia hawa wachezaji na kuwapa muda wa kucheza! After Camp Nou now is the Time of SANTIAGO BERNABÉU 🤩💪
Let’s Goo!!.
Wapwa:Anaandika @officialevodiusoscar_