Hivi ule mchango wa kuichangia YANGA uliishia wapi ?
Jana nilikuwa mimekaa kwenye banda umiza nikiwa natazama mechi kati ya Tanzania Prisons na Yanga. Hapana shaka hii ni mechi ambayo ilikuwa na hisia kubwa sana kuzidi mechi zote ambazo zimechezwa msimu huu kwenye ligi kuu. Ilikuwa mechi ambayo ilionesha namna gani ambavyo mashabiki wa Yanga wana mapenzi makubwa na timu...