Martin Kiyumbi

Mchambuzi
Mchambuzi wa mpira wa miguu, mwenye Shahada ya Ualimu. Martin amejiunga na timu ya kandanda toka mwaka 2017, moja kati ya wachambuzi wakongwe katika familia yetu.
Ligi Kuu

Singida wakanusha habari za KUKIMBIWA na wachezaji.

Kuna habari zilikuwa zimezagaa kuwa baadhi ya wachezaji wa Singida United wameandika barua kwa viongozi wao kuomba kuvunja mkataba kutokana na hali ngumu ya uchumi ndani ya klabu hiyo. Kandanda.Co.Tz iliamua kumtafuta Mkurugenzi Mkuu wa klabu hiyo Festo Sanga kutudhibitishia ukweli wa habari hizi ambazo zinazidi kuenea kwa kasi. Alipotafutwa...
Ligi KuuUhamisho

98% , Chirwa ni mchezaji wa AZAM FC.

Jana kulizagaa habari za Obrey Chirwa kusajiliwa na klabu ya Azam Fc. Tovuti yako ya Kandanda.co.tz iliamua kumtafuta manager wa klabu hiyo ya Azam Fc , Philipo Alando kutudhibitishia ukweli huo. Philipo Alando alipoulizwa kuhusu usajili huo alijibu kwa kifupi kuwa 98% , Obrey Chirwa kasajiliwa na klabu ya Azam...
Ligi KuuUhamisho

Obrey CHIRWA kwenda Azam Fc ni pigo kwa YANGA

Msimu jana ulikuwa mgumu sana kwa Yanga kuanzia ndani mpaka nje ya uwanja. Ilikuwa Yanga ambayo ilikuwa na matatizo mengi sana. Matatizo ambayo yalichangia kwa kiasi kikubwa wao kupoteza ubingwa wao kwa wapinzani wao Simba. Haikuwa Yanga ile ambayo tulikuwa tumeizoea, Yanga ambayo ilifanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu Tanzania...
TetesiUhamisho

Chirwa kutua Azam Fc

Aliyewahi kuwa mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Obrey Chirwa inawezekana akatua katika klabu ya Azam FC. Taarifa za ndani zinasema kuwa mpaka sasa Obrey Chirwa ana nafasi kubwa ya kutua kwenye timu hiyo yenye makazi yake Chamanzi, Dar-es-Salaam. Obrey Chirwa aliachana na Klabu ya Yanga mwishoni mwa msimu uliopita na...
Blog

Natamani kumuona HENRY akiwa kocha bora kama alivyokuwa MCHEZAJI.

Dunia iliwahi kuwa sehemu kubwa ambayo vitu vingi vizuri viliwahi kuishi. Aliwahi kuishi Yesu kwenye dunia hii hii ambayo kila uchwao tunaamka na kukutana na jua. Waliwahi kuishi WAFALME wengi sana, hata MFALME SULEIMAN Aliwahi kuishi kwenye dunia hii. Pamoja na kwamba tunapita ila nafsi yangu inajivunia na Mimi kuishi...
Blog

Wanayanga wanalazimisha kuona wakiwa wamefumba MACHO!

Hakuna mtaji mkubwa duniani kama maarifa, maarifa ndiyo mtaji mkubwa na wa kwanza kwenye dunia hii ambayo taarifa ndiyo mfalme wa mafanikio yote. Huwezi kupata mafanikio makubwa kwenye kitu unachokifanya bila kuwa na "taarifa" na huwezi kufikiria kupata taarifa kama huna "maarifa". Ni vitu viwili muhimu sana ambavyo vinategemeana sana...
Blog

Niyonzima atemwa rasmi

Kiungo wa klabu ya Simba, Haruna Niyoñzima, ametemwa rasmi katika kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda, baada ya kuitwa kwa miaka 11 mfululizo. Kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda kinajiandaa na mechi za kufuzu michezo ya Afcon. Kutemwa kwake kumesababishwa na yeye kutopata nafasi ya kucheza katika klabu...
Ligi Kuu

Hapana! Zahera amefikia pabaya.

Niliwahi kuandika kuwa ni ngumu kwa Yanga kubeba ubingwa wa ligi kuu ikiwa na mshambuliaji aina ya Makambo. Na hii ni kwa sababu anakosa nafasi nyingi sana za wazi. Na kibaya zaidi hakuna mtu ambaye anaweza kuwa kama mbadala, benchi la Yanga lina ufinyu wa washambuliaji, ufinyu ambao unamfanya Makambo...
Uhamisho

Safari ya Ulimwengu kwenda Yanga yaiva!

Mshambuliaji wa zamani wa Tp Mazembe ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) amevunja rasmi mkataba wake na klabu ya Al Hilal ya Sudan. Imeripotiwa Mshambuliaji Thomas Ulimwengu amevunja mkabata wake na klabu ya Al Hilal ya Sudan akiwa amedumu kwa miezi mitano tu. Kabla...
1 55 56 57 58 59 79
Page 57 of 79