Kuelekea mchezo wao wa marejeano wa Caf Confederation Cup dhidi ya KCCA FC ya Uganda kesho Jumamosi, nahodha wa Mtibwa Sugar FC, Shaaban Nditti amekiri watalazimika kucheza 'kufa na kupona' ili kupindua matokeo ya 3-0 na kufuzu kwa hatua ya mwisho kuwania nafasi ya kufuzu kwa hatua ya makundi.
Mabingwa wa soka nchini Simba Sports Club wameanza vibaya mchezo wa raundi ya kwanza wa ligi ya mabingwa Afrika baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Nkana ya Zambia mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Nkana mjini Kitwe. Simba ambayo iliyoingia kwa kujiamini hasa baada ya raundi ya awali...
Kiungo mshambulizi wa Mtibwa Sugar FC, Haroun Chanongo amesema wanafahamu wanakabiliwa na kazi kubwa dhidi ya KCCA FC katika mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya Caf Confederations Cup.
Kocha wa makipa wa timu ya soka ya Mtibwa Sugar Patrick Mwangata ameeleza kwamba wanaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa hatua ya kwanza ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya KCCA ya Uganda Disemba 15 mwakahuu. Mwangata amesema wameshaanza mazoezi kwa siku ya nne sasa nawanacholenga kwa sasa ni...
Wakata miwa wa Mtibwa Sugar wameendeleza ubabe wao katika michuano ya Kimataifa baada ya kutoa kipigo ugenini na kufanikiwa kuingia raundi ya kwanza katika michuano hiyo ya Shirikisho Africa. Mtibwa Sugar imefanikiwa kuifunga Northern Dynamos kwa bao moja kwa sifuri ugenini hivyo kufanikiwa kuwatoa Washelisheli. Haruna Chanongo ndie mfungaji wa...
Klabu ya soka ya Mtibwa Sugar imewashukuru watanzania waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Azam Complex kuiunga mkono wakati wa mchezo wao wa shirikisho Afrika dhidi ya Northern Dynamo ya Ushelisheli. Thobias Kifaru Ligalambwike ambaye ni Afisa habari wa Mtibwa Sugar amesema wameweza kufikia malengo na kupeperusha vyema bendera ya...
Klabu ya soka ya Mtibwa Sugar ‘WanaTam Tam’ ya Manungu Turiani mkoani Morogoro wameanza vyema michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Northern Dynamo ya nchini Ushelisheli. Mtibwa Sugar wakicheza kandanda safi kuanzia sekunde ya kwanza ya mchezo katika...
Miaka 14 imepita bila wao kufuzu kucheza mechi za kimataifa. Leo hii Mtibwa Sugar wanaenda kucheza mechi yao ya kimataifa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 14. Mtibwa Sugar wamechagua uwanja wa Chamazi kama uwanja wao wa nyumbani katika mechi hizi za kimataifa. Na mechi yao ya kwanza itawakutanisha...
Baada ya miaka 14 Mtibwa Sugar inatarajiwa kurejea katika michuano ya Kimataifa na mara hii itakuwa ikiumana na Northern Dyamos ya Ushelisheli katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika hatua ya awali. Mchezo huo wa Kimataifa Utafanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamazi Jijini Dar es Salaam ambapo tayari...