Sambaza....

Wakata miwa wa Mtibwa Sugar wameendeleza ubabe wao katika michuano ya Kimataifa baada ya kutoa kipigo ugenini na kufanikiwa kuingia raundi ya kwanza katika michuano hiyo ya Shirikisho Africa.

Mtibwa Sugar imefanikiwa kuifunga Northern Dynamos kwa bao moja kwa sifuri ugenini hivyo kufanikiwa kuwatoa Washelisheli.

Haruna Chanongo ndie mfungaji wa bao hilo pekee katika dakika ya 68 na mpaka mpira unamalizika Mtibwa Sugar wakiondoka wababe katika uwanja wa ugenini.

Mtibwa Sugar imefanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo kwa jumla ya ushindi wa mabao matano kwa bila, baada ya kupata ushindi mnono wa mabao manne kwa sifuri katika uwanja wa Chamanzi Complex.

Kwa matokeo hayo Mtibwa Sugar wanakwenda kukutana na KCCA ya nchini Uganda katika hatua inayofuata ya michuano hiyo ya Shirikisho Africa.

Sambaza....