Shirikisho Afrika

Michuano ya AFCON yasogezwa mbele kupisha Ramadhan.

Sambaza kwa marafiki....

Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limekubali kusogeza mbele tarehe ya kuanza kwa michuano ya Mataifa Afrika ili kupisha mwezi mtukufu wa Ramadhan unaotazamiwa kuanza mwezi Mei.

Michuano hiyo ambayo itachuku wiki nne sasa itaanza Juni 21 na fainali zake zitafanyika Julai 19 wakati awali zilipangwa kufanyika kuanzia June 15 hadi Julai 13 mwaka huu nchini Misri.

“Maamuzi haya yamekwenda sambasamba na ombi la Morocco, Tunia and Algeria ambao wameomba wachezaji wao wapate mapumziko baada ya mwezi Ramadhan kumalizika,” amesema Mwenyekiti wa mashindano ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Misri Mohamed Fadl.

Wakati huohuo CAFimethibitisha kuwa Droo yakupanga makundi kwa timu zitakazoshiriki itapangwa April 12 mwaka.

Tafadhali tumia viungo rasmi kusambaza habari zetu. Facebook, Twitter au Barua Pepe. Kama utataka kutumia habari zetu tuandikie kupitia habari@kandanda.co.tz