Sambaza....

Kiungo mshambulizi wa Mtibwa Sugar FC, Haroun Chanongo amesema wanafahamu wanakabiliwa na kazi kubwa dhidi ya KCCA FC katika mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya Caf Confederations Cup.

Timu hizo mbili ( KCCA na Mtibwa) zinataraji kupambana wikend hii jijini Kampala na Chanongo anaamini ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya mwisho ya mtoano wanatakiwa kuhakikisha wanafunga katika mchezo wa wikend hii.

“ Ni mechi ngumu tuinakwenda kucheza ugenini, lakini tutapambana kuhakikisha tunafunga goli au magoli ya ugenini.” Anasema Chanongo mfungaji wa bao pekee la Mtibwa katika ushindi wa 1-0 ugenini vs Dynamo ya Shelisheli.

“ KCCA ni timu nzuri, wana uzoefu mkubwa katika michuano ya Caf lakini hii si sababu ya kuwahofia. Tutapambana ili kushinda na kusonga mbele.”

Sambaza....