Kapombe
Ligi Kuu

Kapombe ni pengo, lakini..!

Sambaza....

KWA mara nyingine mlinzi ´kiraka´ wa klabu ya Simba SC na timu ya Taifa ya Tanzania ( Taifa Stars), Shomari Kapombe atalazimika kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kuumia kifundo cha mguu Alhamis iliyopita.

Kapombe alikanyaga vibaya mpira katika mazoezi ya timu ya Taifa wakati wakijiandaa na mchezo wa kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika dhidi ya Lesotho huko jijini Bloemfontein Afrika Kusini na taarifa za awali zinadai huenda ikamchukua wiki nane hadi 12 kabla ya kurejea uwanjani.

Kwa misimu yake miwili ya mwisho akiwa Azam FC ( 2015/16 & 2016/17), Kapombe alikosa michezo mingi kutokana na majeraha na miaka miwili iliyopita alilazimika kupelekwa Afrika Kusini kwa matibabu makubwa ya tumbo.

Agosti 8, 2017 wakati aliposajiliwa Simba kwa mara ya pili, Kapombe alipata majeraha makubwa ya mguu na alilazimika kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi minne. Kwa ufupi mlinzi huyo wa pembeni anapitia nyakati ngumu kwa miaka mitatu sasa katika kazi yake.

Ni changamoto ambazo mtu yeyote anaweza kuzipitia, na wakati huu akiwa nje ya kikosi klabu sambamba na Shirikisho wanapaswa kumsaidia ili apone haraka.

Kumekuwa na mitazamo tofauti tangu kuumia kwa Kapombe- hasa kwa watu wa Simba ambao sasa wanataka kuona timu yao ikiingia haraka sokoni katika usajili huu wa dirisha dogo na kusaini mlinzi wa kulia.

Sioni kama ipo sababu ya Simba kukimbilia sokoni na kuacha kutilia mkazo matibabu ya Kapombe. Simba inaweza kuendelea kuwatumia Mghana, Nicolaus Gyan na kiraka mwingine, Erasto Nyoni katika beki ya kulia na si kusaini mchezaji mpya.

Wawili hao ( Gyan na Nyoni) walifanya vizuri msimu uliopita katika nafasi ya mlinzi wa kulia wakati Kapombe akiwa na majeraha hata baada ya kupona kwake mwezi Disemba 2017.

Ni suala la kocha Mbelgiji, Patrick Aussems kuhakikisha walinzi hao Wawili au Paul Bukaba na Yusuph Mlipili wanafanya vizuri na kuziba pengo la Kapombe kwasababu hilo ni jukumu lake.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x