Yanga wamesema wapo tayari kumpokea mchezaji wake huyo baada ya maamuzi ya kamati ya sheria na hadhi ya wachezaji kumhalalisha kuendelea kuwatumikia Wananchi.
Mara ya mwisho Feisal kuitumikia Yanga ilikua katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania uliopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa na kuisaidia timu yake kupata ushindi wa bao moja kwa sifuri.
Lakini Fei wa sasa amereje upya kwenye form yake nadhani ndio muda wa kuondoka sasa, kiufundi anachopaswa kufanya ni kuongeza uwezo wa kutafsiri mahitaji ya mchezo kutokana na muda na tukio.