Feisal Salum
Tetesi

Fei Toto kwenda Azam FC

Sambaza....

Baada ya kuendelea kufanya usajili kwa ajili ya kujiimarisha na ligi kuu Tanzania bara msimu ujao kwa kuwaleta wachezaji nyota ndani ya kikosi cha Azam FC.

Mpaka sasa hivi Azam FC wamefanikiwa kupata saini ya kiungo aliyekuwa anachezea Kagera Sugar Awesu Awesu , kiungo ambaye alikuwa anawaniwa na mabingwa wa kihistoria Yanga.

Yanga pia walikuwa wanamwania Ally Niyonzima kiungo mahiri kutoka Rayon Sports ya Rwanda lakini Azam FC waliwawahi Yanga na kumsajili kiungo huyo na kuwa ni usajili wa pili baada ya Awesu Awesu.

Baada ya kuwazidi Yanga kwenye sajili hizo mbili timu ya soka ya Azam FC imeamua kuingia kwenye kikosi cha Yanga ili kumsajili kiungo wao nyota Faisal Salum Fei Toto .

Taarifa za ndani zinadai kuwa Azam FC imeshaanza mazungumzo na mchezaji huyo , mazungumzo ambayo yanaonekana kufikia katika sehemu ambayo ni nzuri kwa pande zote mbili.

Sambaza....