Wengi tunawahukumu Rivers kwa tulivyowaona mara ya mwisho walivyocheza na Yanga. Kisha tunapima kuimarika kwa Yanga. Tukitoka hapo moja kwa moja tunaona Rivers kashatolewa na Yanga kasonga mbele
Tangu ilipochukua ubingwa mwaka 2018 bado haijawa tena tishio sana na kama Simba watakwenda Tunisia kucheza nao robo fainali itakua ni mara yao ya kwanza kwa miaka ya hivi karibuni
Simba itampasa kuchanga vyema karata zake katika mchezo wa kwanza kama kweli wanataka kwenda nusu fainali kwani wataanzia nyumbani mchezo wa kwanza na kumalizia ugenini mchezo wa mwisho.
Katika mshindano ya Afrika, Club Vita ilishawahi kuwa bingwa wa Klabu bingwa Afrika mara moja mwaka 1973, na mwaka huu imefika fainali katika mashindano ya shirikisho Afrika. Na katika mashindano ya Afrika Mashariki “Kagame Cup” ilishawahi kushika nafasi ya 3 mwaka 2012.