Blog

YANGA wameshafungwa 3-0 na SIMBA

Sambaza....

 

Maisha yanatupa nafasi muda kutupa nafasi sisi wanadamu. Nafasi ambazo ndizo huwa daraja kubwa kwetu sisi kufikia mlima mafanikio. Mlima ambao ni mgumu sana kuupanda.

Na ndiyo mlima pekee ambao kila mwanadamu anaupanda, kila uchwao maisha hutoa ruhusa kwa muda ili muda utupe sisi nafasi za kutumia kuupanda huu muda.

Viongozi wa Simba walipotembelea Bunjui

Tofauti yetu huanzia hapa (namna tunavyofikiria njia za kufikia kilele cha mlima mafanikio). Kila mmoja wetu hupewa muda sawa kabisa wa kutumia kupanda huu mlima. Lakini tofauti huanzia kichwani.

Tofauti ambayo hutengeneza masikini na tajiri. Hapa ndipo huwa tunafanikiwa kwa kiasi kikubwa kupata aliyefanikiwa na ambaye hajafanikiwa , na bila shaka mtu ambaye amefanikiwa ndiye yule ambayo anayetumia nafasi yake vizuri aliyopewa na bwana muda.

Na huyu aliyefanikiwa hutazamwa zaidi kama kitabu ambacho hutumiwa na watu wengi kupata mbinu za namna ya kufanikiwa. Wengi huwa hawamtazami sana ambaye hajafanikiwa, na huyo ambaye hajafanikiwa huwa hajitazami sana yeye huwa anamtazama sana aliyefanikiwa.

Ndicho kitu ambacho kilitokea kwa Dkt. Mshindo Msolla, mwenyekiti wa klabu kubwa sana hapa nchini ya Yanga. Mtu ambaye anajua kabisa klabu yake haina mafanikio makubwa sana kiasi cha kushindwa kulipa mishahara ya wachezaji wake.

Hatamani eneo ambalo Yanga ipo, anaumia kuiona Yanga ikiendeshwa ilimradi siku ziende. Anaumia sana, uso wake unaonesha namna anavyoumia. Macho yake yanatamani kutoa machozi kutokana na maumivu ambayo moyo wake yanaupata.

Viongozi wa Yanga wakiwa katika eneo walilopewa na Manji, ambalo sasa ni eneo la serikali.

Amekuwa kiongozi muazi , hajatamani kabisa kujikweza ilihali hana kitu. Anaumia kutokuwa na kitu na anatamani Siku moja apate hicho kitu . Na kwa kinywa chake kabisa kuna magoli matatu (3) ambayo ameyaona yeye kama yeye amesbafungwa na Simba mpaka sasa hivi.

Mdomo wake unakiri kabisa kitendo cha Simba kuwa na uwanja wake wa mazoezi ni kitendo ambacho ni cha maendeleo , kitendo ambacho na wao kama Yanga wanatamani sana kuwa nacho.

Inawezekana kinywa chake kimekiri kuhusu kiwanja pekee , lakini kimegoma kukiri kuhusu mishahara , hili ni goli la pili ambalo Yanga wamefubgwa na Simba mpaka sasa hivi , Yanga hawalipi mishahara ya wachezaji kwa wakati ukilinganiaha na Simba.

y

Kwa Simba kuwa na Uwanja , kulipa mishahara mapema kunatokana na maamumizi ambayo Simba waliamua kuyafanya , maamuzi ya kuingia kwenye mabadiliko ya uendeshaji wa timu.

Dkt.Mshindo Msolla amesema kufikia mwezi wa tano mwakani Yanga wataingia kwenye mabadiliko ya mfumo wa uendeshwaji wa timu na hapa ndipo goli la 3 ambalo Yanga wamefungwa na Simba.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x