George Mpole akishangilia na wachezaji wa Stars wakishangilia goli katika mchezo dhidi ya Niger lililofungwa na George Mpole
AFCON

Afcon!? Twenzetu Tena na Hawahawa Tulionao!

Sambaza....

Bendera ya Tanzania  ipo kwenye mikono yenu, leo ni zamu yetu kwenye dakika 90 zenye alama moja ya ushindi kuitafuta AFCON dhidi ya Algeria Usiku wa leo.

Ndio ni hii Taifa Stars ambayo tulicheza AFCON 2019 baada ya kushinda mchezo wetu dhidi ya Uganda ndani ya Mkapa Stadium leo kwanini isiwezekane? Inawezekana kwa 100%.

Mbwana Samatta! Umeamua mechi nyingi za Klabu zako ulizocheza bado haikutosha umefanya hivyo mara kadhaa ndani ya Timu ya Taifa hivyo leo tena Watanzania tumekukabidhi jukumu hilo la kutupa alama moja.

Simon Msuva mfungaji wa bao pekee dhidi ya Uganda katika mchezo wa ugenini.

Simon Msuva! Kwa sasa wewe ni mfano mzuri kwa vijana wengi kuwa ukipewa nafasi Timu ya Taifa basi itumia vyema na umefanya hivyo, uliamua mechi nyingi hapo nyuma basi na leo tunasubiri ufanye hivyo.

Novatus Dismas! Wewe umeonyesha uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani na kutatekeleza majukumu yako kwa usahihi, hivyo basi nenda kawaoneshe Algeria kuwa haikuwa bahati mbaya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kibu Denis! Endeleza kile ulichokianza msimu uliopita Tanzania haina mashaka na wewe. Bakari Nondo endelea kuimarisha ulinzi salama leo ukimshirikisha Dickson Job, Kennedy Juma au Ibrahim Bacca.

Ibrahim Bacca na Mudathir Yahya wakimdhibiti mchezaji wa Uganda.

Hapa tunazungumza safari ya ushindi tu, hapa tunahitaji Bendera ya Tanzania  ipepee Kimataifa lakini lazima tupate ubora wa Mudathir, Mzamiru, Bajana, Mkude, Sure Boy nyuma ya washambuliji wetu na mbele ya ukuta wetu.

Ndio! Hatuna rekodi nzuri dhidi yao lakini leo ni nafasi ya kuweka heshima na kupata rekodi nzuri dhidi yao, sisi na wao tunakutana kama wimbo wa Marioo na Alikiba usemavyo “sisi ni people tutakutana” huo ndio mpira.

Muda wa kupeperusha bendera ya Tanzania yenye rangi nne zenye thamani ya ushindi siku zote! Ndio hili Taifa ambalo lina mlima mrefu na Ziwa lenye kina kirefu kuliko yote Afrika, hivyo leo tunataka alama moja pia ili kucheza mashindano ya Afrika.

 


Sambaza....