Sambaza....

Timu ya soka ya Al Ahly imejiwekea rekodi ya kipekee baada ya kuifunga Al Masry kwa mabao 2-0 katika mchezo wa mwisho wa ligi hapo Jana.

Mabingwa hao wa kihistoria wa Misri wamefikisha alama 88 ndani ya michezo 34 ya ligi wakiipiku rekodi ya mahasimu wao Zamalek ambao waliwahi kufikisha alama 87 katika msimu wa mwaka 2014/15.

Al Ahly wameweka rekodi hiyo wakicheza michezo 34 pekee yake ambayo ni pungufu ya michezo minne kwani Zamalek waliweka rekodi hiyo baada ya kucheza michezo 38 kipindi hicho ligi ikiwa na timu 20 tofauti na timu 18 za sasa.
Mabingwa hao mara nane wa Afrika wameweka rekodi nyingine mbili muhimu katika ligi hiyo ikiwemo ile ya kushinda michezo 28 katika msimu mmoja wakivunja rekodi yao we wenyewe ya mwaka 1974/75 na ile ya Zamalek ya mwaka 2014/15 ambapo walishinda michezo 26.

Aidha mabao 75 waliyofunga msimu huu yamewasaidia kuipiku rekodi ya Al-Tarsana waliyoiweka msimu wa 1963/64 kwa kufunga mabao 71 ndani ya msimu mmoja.

Ligi hiyo imemalizika jana ambapo kiatu cha mfungaji bora kimeenda kwa Mshambuliaji wa Al Ahly Walid Azaro mwenye umri wa miaka 22 ambaye amefunga mabao 18 na kuwa mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kutwaa kiatu hicho tangu mara ya mwisho alilofanya hivyo Flavio Amado raia wa Angola mwaka 2007 pamoja na Mnigeria John Utaka ambapo sasa Azaro ambaye ni raia wa Morocco anakuwa mgeni wa kwanza kufunga mabao mengi katika ligi hiyo.

Sambaza....