Blog

Burundi wametufiundisha kuhamia Digitali, Tusichelewe tuhame nao

Sambaza....

Ni mchezo wa tatu sasa kocha Ettiene Ndailagije anazidi kufanya vema katika mechi anazoinoa stars akisimama kama kocha mkuu, mechi ya kufuzu michuano ya CHAN pamoja na hii ya kuwania nafasi ya kuingia katika makindi ya timu zitakazo wania nafasi ya kwenda kombe la dunia 2022.

Ingawa ni mapema kuhukumu au kusifia kumekuwa na mabadiliko makubwa hasa kwa wachezaji wale wale waliotumiwa na makocha wengine na Stars ikafanya vibaya, kwa sasa timu inaweza kucheza kwa uhuru, ikamiliki mpira na ikawa na utilivu licha ya kuwa ipo ugenini. Katika michezo mitano ya ugenini Stars chini ya kocha Mnigeria Emmanuel Amunike iliweza kupata sare mbili na kupoteza tatu ukitoa mechi za Afcon ambazo tulivurunda.

Kuna jambo kufanya kwa Ettiene na benchi lake yaani kuunganisha wachezaji wanaocheza nje na wachezaji wa ndani ili kupata timu moja. Katika mchezo wa jana ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Mbwana Samatta, Simon Msuva, Himid Mao na Faridi Malik kupewa majukumu wanayotakiwa yafanywe kulingana na mahitaji ya mbinu za mwalimu, huku wakifika kambini siku moja kabla ya mchezo.

Kwa sasa baada ya kukaa nao kwa siku tatu tutarajie mabadiliko makubwa ya kimuunganiko na kimbinu. Mbinu za Ettiene ni mbinu sahihi kwa mechi sahihi huwenda tatizo likabaki kwa wachezaji wetu wanapozidiwa maarifa na wachezaji wa timu pinzani wenye uzoefu katika michezo mikubwa ya kimataifa.

Watanzania wengi wanaamini kuwa baada ya kupata sare ya moja moja pale uwanja wa mashuja nchini Burundi kazi imeisha, lakini bado shilingi imesimama. Matokeo yanaweza kupatikana popote kama tu Walivyo ondoshwa Kenya nchini kwao katika mchezo kutafuta tiketi ya kushiriki CHAN, ama jinsi Simba walivyo ondoshwa na UD Songo.

Soka la kiafrika ukishindwa kushinda nyumbani basi umetolewa, stars wanapaswa kuhakikisha wanashinda nyumbani. Mtazamo wa Burundi kuja kushambulia si wa kubashiri ni mbinu za wazi watakazo tumia maana tayari wamepoteza nyumbani, kusipokuwa na mipango imara wanaweza kuamua kuja kufia Tanzania ingawa historia inawahukumu katika takwimu.

Udhaifu wa Burundi umeonwa na uimara wao pia tumeuona kwa kuwa silaha yao ni kufungukia pembeni basi kunahaja ya kufanya mabidiliko makubwa sana ya kiufundi huku wakiwekewa ulinzi madhubuti eneo la kati kama ilivyokuwa nchini kwao. Na kuhakikisha Kipa wa Stars anaimarisha mawasiliano na walinzi huku akiongeza tahadhari na kupunguza kujiamini kupita mipaka yake na mbinu za mwalimu.

Kwa sasa kisaikolojia Burundi baada ya kutofanikiwa baada kufanya hujuma nchini kwao ili waitoe Tanzania mchezoni waishajifunga uwanjani, baada kufanya yote yale kwenye eneo walilo na uhuru mwingi walipaswa kushinda asubuhi tu, kwa kutofanikiwa wamejinunulia kesi watakapokuja Tanzania.

Muda wa kuhama kutoka analogia kwenda digitali umefika, Tanzania wanapaswa kujua mpira ni maisha na kile walichokifanya Burundi ndio mpira wenyewe wa kidigital….na wanapaswa kuhama kutoka huko analogia na kuja kuendana na kasi ya mifumo ya kisasa.

Kisaikolojia Burundi wameishashindwa kwao, wanapofika ugenini watakuwa wakiishi kwa kwa mashaka kama mwananchi aliyepeleka chakula cha mfungwa gerezani huku kikiwa kwenye mfuko wa plastiki (Rambo). Hivyo wanapaswa kuvurugwa nje ya uwanja na ndani ya uwanja kazi iishe.

Na Hebron M Admin

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x