Sambaza....

Tanzania inatarajia kupokea ugeni wa wajumbe wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kwa ajili ya kukagua miundo mbinu pamoja na kupanga makundi ya michuano Mataifa Afrika chini ya umri wa miaka 17 itakayofanyika mwakani hapa nchini.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya michezo Yusuph Singo amesema ugeni huo inatarajiwa kuwasili Disembe 16 ambapo utakagua viwanja vya mazoezi, hotel, hospitali, viwanja vya mashindano pamoja na kupanga makundi shughuli ambayo itafanyika Disemba 20 kabla ya kuondoka nchini Disemba 21.

“Ni kweli tunataraji kupokea ugeni kutoka CAF ambao wataingia nchini tarehe 16 na watakaa hadi tarehe 21, watakuja kufanya ukaguzi wa maeneo mbalimbali kwa ajili ya michuano ya AFCON U17 lakini Jukumu kingine watakalokuwa nalo ni kufanya droo kwa maana ya kwamba kupanga makundi kwa ajili ya michuano hiyo na drop hiyo itafanyika tarehe 20,”

“Programu yao kamili wataituma TFF kuonesha katika siku hizi Tano watakuwa na vitu gani vingine zaidi, so far tumepokea majina sita lakini umekuwa tukifanya mawasiliano ya karibu na huenda wakaongezeka maana mara nyingi timu zile ambazo zinashiriki huwa zinakuwa na wawakilishi,” Singo amesema.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza April 14 Hadi 28 ambapo timu zilizofuzu ni pamoja na wenyeji Tanzania, Morocco, Senegal, Guinea, Nigeria, Angola, Uganda na Cameroon

Sambaza....