Sambaza....

Klabu ya Chelsea imesema itapitia tena video inaonesha mashabiki wake wakimtupia maneno winga wa Manchester City Raheem Sterling, maneno ambayo yanadhaniwa kuwani ya kibaguzi wakati wa mchezo wao jana Jumamosi.

Katika video hiyo iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii inaonesha Mashabiki wa Chelsea wakitoa maneno makali kwa Sterling wakati akienda kuokota mpira nyuma la lango la Chelsea.

Mpaka sasa hakuna watu waliokamatwa kutokana na video hiyo kuwekwa mitandaoni lakini tayari Polisi wameshatoa waraka kwamba wanaona kuna umuhimu wa kuiangalia video hiyo ili kujithibitishia kama kweli kulitokea kitendo chochote cha ubaguzi wa rangi.

Pamoja na hilo pia Chelsea wametoa tamko likisema kuwa “Tunaufahamu wa video hiyo kuwepo mtandaoni ikisemekana kuwa kuna vitendo vya ubaguzi vilivyofanywa kwa mchezaji kwenye uwanja wetu wa Stamford Bridge Jumamosi,…….. Tutaipitia tena video hiyo ili kufahamu kama kuna kosa lolote limefanyika,”.

Katika mchezo huo wa ligi kuu England, Chelsea waliivunja rekodi ya Manchester City yakutofungwa, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Kiungo Ngolo Kante na beki David Luiz.

Sambaza....