Sambaza....

Taarifa za ndani kutoka kwa Mabingwa wa kandanda nchini Kenya Gor Mahia ni kuwa wanajiandaa na kuondoka kwa Kocha mkuu wa Dylan Kerr.

Gor wameanza maandalizi hayo baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa kocha huyo ambaye amewapa mataji mawili ya ligi huenda akaondoka na kutafuta sehemu yenye malisho mazuri zaidi.

“Haitakuwa taarifa ya kushangaza kama ataondoka, ameshawahi kujiuzulu mara kadhaa katika maeneo mengine aliyofanya kazi, ameshajijengea jina hapa ni suala la muda tu yeye kuondoka na kutafuta sehemu nzuri kwake, tushajiandaa kwa hilo,” mtandao wa kahawatungu umemripoti mmoja wa viongozi wa ndani wa Gor Mahia.

 

Kerr aliwahi kuudumu kama kocha wa Klabu ya Simba kabla ya mwaka 2017 kujiunga na Gor Mahia na amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake lakini tayari dalili za kuondoka klabuni hapo zinaonesha wazi.

Hajarudi na timu kutoka nchini Uingereza ambapo walicheza na Everton katika mchezo wa kirafiki kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya unaotarajiwa kuanza mapema mwakani.

Sambaza....