Blog

Ettiene ni Klop asiyekuwa na Alexander Anorld pamoja na Robertson

Sambaza....

Mfumo wa 4-3-3 ndiyo mfumo mama wa kocha wa Liverpool Jurgen Klopp. Mfumo ambao hubeba mabeki wanne (Alexander Anorld , Matip, Van Djik na Robertson). Ukuta huu kwa mbele yake huwa na viungo watatu (Fabinho , Wijnaldum na Henderson) huku mbele kukiwa na ule utatu mtakatifu (Salah, Mane na Firmino).

Katika timu ya Jurgen Klopp , hakuna kiungo wa eneo la Kati mwa uwanja ambaye hutengeneza nafasi nyingi za magoli. Mfano kwa pamoja Fabinho , Wijnaldum na Henderson kwa msimu huu nafasi ambazo wametengeza hazizidi tano. Henderson katengeneza nafasi mbili , huku Fabinho na Wijnaldum wakiwa wametengeza nafasi moja moja kila mmoja.

Kiungo ambaye anaongoza kutengeneza nafasi nyingi za magoli msimu huu kwa upande wa Liverpool ni Alex Oxlaide Chamberlaine ambaye katengeneza nafasi nne. Na huyu mara nyingi hutokea Benchi huwa haanzi mara kwa mara. Kwa hiyo Jurgen Klopp haitaji kiungo mbunifu sana kwenye timu yake.

Sasa kipi ambacho huwa silaha ya Jurgen Klopp ? Silaha kubwa ya huyu Mjerumani ni pembeni mwa uwanja. Huku ndiko kulipo sehemu ambayo hutumia kuwaangamiza wapinzani wake mara nyingi tu.

Klop (Kocha wa Liverpool)

Ni jinsi gani huwaangamiza ? Huwa anahakikisha timu pinzani inalazimishwa kutengeneza uwazi eneo la pembeni mwa uwanja. Ambapo washambuliaji wa Liverpool, Saido Mane au Mohamedd Salah huwa wanaingia ndani wakitokea pembeni mwa uwanja, wakifanya hivo mabeki wa timu pinzani hujikuta wanawafuata na kuacha uwazi eneo la pembeni.

Uwazi ambao mara nyingi hutumiwa na mabeki wa pembeni Alexander Anorld upande wa kulia pamoja na Robertson upande wa kushoto. Hawa hutengeneza nafasi nyingi za magoli kupitia eneo la pembeni mwa uwanja. Mfano kwa msimu huu kwa pamoja wametengeza pasi 30 za magoli.

Hiki kitu kipo pia kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ambayo mara nyingi hutumia mfumo wa 4-3-3 chini ya mwalimu Ettiene , viungo wa Kati wa timu ya taifa siyo wabunifu kama walivyo viungo wa Kati wa Liverpool. Mara nyingi huwa tunajikuta tunategemea pembeni mwa uwanja..

Cha kusikitisha pembeni mwa uwanja mabeki wetu wa pembeni huwa hawatengenezi sana kwa wingi nafasi za magoli. Ni mara chache sana kwa beki wa pembeni kutoa Pasi ya mwisho ya goli. Kiumbo timu ya taifa inaumbo la Liverpool lakini inakosa mabeki wa pembeni wenye uwezo wa kutoa pasi za mwisho kama Alexander Anorld na Roberstson.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.