Sambaza....

Kampuni ya Promosheni ya ngumi HB SADC imetambulisha rasmi pambalo la ngumi ambapo litaambatana na “Royal Tour” litakalofanyika mkoani Mwanza.

Wakiongea mbele ya Waandishi wa habari kutambulisha pambano hilo ambalo litaambatana na utalii wa ndani litawakutanisha bondia Mtanzania Fadhili Majiha na mpinzani wake atatoka nchini Ufilipino.

 

Akitambulisha pambano hilo mkurugenzi wa HB SADC Hamis Kumbucha alisema “Safari hii tumekuja tofauti katika boxing, tunakuja na utaalii na boxing,” alisema na kuongeza;

“Tunaanzia mkoani Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla kwasababu tunajua watu wa Mwanza wanapenda sana ngumi lakini hawakuwahi kupelekewa mapambano yakueleweka.”

“Sisi kama HB tunapatikana katika nchi zote za SADC lakini tunafanya shughuli nyingine. Tumeamua kuingia kwenye mchezo wa ngumi na kuacha michezo mingine kwasababu tunaona ndio mchezo sahihi zaidi na tunataka kuuendeleza mchezo huu zaidi,” alimalizia Hamis.

Bondia namba moja nchini katika uzito wake Fadhili Majiha amesema anafurahi kupata fursa hiyo na amejiandaa vyema kuelekea pambano hilo.

Tony Rashid na Mfilipino Renz Rosia watagombani mkanda wa UBO katika uzito wao na pambano hilo linatarajiwa kufanyika mkoani Mwanza September 30 ya mwaka huu.

“Nawashukuru sana HB kwa kuniandalia pambano hili, mimi ni bondia mkubwa Tanzania lakini sikuwa nimepata nafasi sana. Nimepata mikanda mingi nje ya nchi Kenya na Afrika Kusini nikiwapiga Mwingireza na Muindonesia.”

Mkanda utakaogombaniwa September 30.

“Nashukuru Mungu kwa zawadi hii ya mikono na hiki kipaji, nawajua Wafilipino ni wagumu sana lakini nimejiandaa vyema. Watanzani na watu wa Mwanza mje kwa wingi kunisapoti siku ya pambano,” alimalizia Majiha.

Pia kuelekea pambano hilo litakalofanyika mkoani Mwanza Rock City Mall litasindilizwa na mapambano mengine madogo yatakayofanyika Burigi Karagwe kati ya September 25 na 26 mwaka huu.

Sambaza....