Ligi

Infantino afurahia mabadiliko TFF

Sambaza....

Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF, ndugu Wallace Karia, amemkabidhi kinyago kilichochongwa Tanzania rais wa Shirikisho la soka Duniani FIFA Giann Infantino aliyekuwa nchini kuendesha mkutano wa FIFA wa maendeleo ya mpira ujulikanao (Fifa football executive summit)

Image result for infantino kinyago

Mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere international convention centre, ambapo rais huyo wa Fifa alielezea imani yake kwa uongozi wa TFF pamoja na serikali ya awamu ya tano ya Tanzania

Akiongea katika mkutano huo, Infantino alisema kuwa “Tupo hapa kwa ajili ya kushirikiana, kusaidiana na kuunganisha nguvu na TFF pamoja na serikali ili kuhakikisha tunafikia malengo”

“Tunataka kubadilisha mambo na kufikia njia sahihi, kwenda katika mabadiliko na baadae mafanikio” alisema Infantino

Pia rais huyo alioneshwa kukerwa na vitendo vya rushwa huku akisisitiza kupigwa vita masuala hayo na kusema kuwa ni chanzo cha kuharibu mambo mengi ya maendelo ya soka

“Tunapiga vita na tutaendelea kupambana na suala hili, kwa sasa tunajua kinachoingia kinatoka wapi na pia kinachotoka kinaelekea wapi”

“Fedha za Fifa zitumike kwa maendeleo ya mpira na sio vinginevyo” alisisitiza Infantino

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x