Mlinzi wa Simba Tairone Santos akipambana na Ditram Nchimbi wa Yanga
Ligi

Hii ndio Derby ninayoijua mimi

Sambaza....

January 4 imeshapita tayari na mchezo wa watani wa Jadi kati ya mwenyeji Simba na Yanga umemalizika kwa sare ya mabao mawili kwa mawili, huku Yanga wakionekana kufanya “wonders” mbele ya mashabiki yao wachache waliojitokeza uwanja wa Taifa.

Baada ya kuongoza bao mbili Simba sc kupitia kwa Meddie Kagere na Deo Kanda waliona wamemaliza mchezo na kuanza kujisahau. Lakini Yanga kupitia wazawa Balama Mapinduzi na Mohamed Issa Banka waliwaongoza Yanga kufanya “Comeback” ndani ya dakika 7 tu na hivyo kumaliza mchezo kwa sare ya bao mbili kwa mbili.

Tazama hapa picha katika mchezo huo uliokua mtamu kwelikweli.

Aishi Manula mlinda mlango wa Simba ambae mashabiki wanamlaumu kwa kuwarudisha Yanga mchezo kwa kuruhusu magoli ya kizembe

 

Ally Sonso akianzisha mashambulizi kutoka katika eneo lake
Mzamiru Yasin akimuacha chini Haruna Niyonzima
Manahodha wawili walipokutana, huku Papy akimuonyesha kazi Tshabalala
Deo Kanda “mtaalamu”
Ditram Nchimbi “Duma”
Balama Mapinduzi akiachia fataki na kufungs bao la kwanza kwa Yanga
Mohamed Hussein “Tshabalala”
Wachezaji wa Simba wakishangilia goli la kwanza liliofungwa na Meddie Kagere
Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli la pili lililofungwa na Mo Banka

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.