Mataifa Afrika

Jionee Rais wa FECAFOOT akifanya mazoezi na timu ya Taifa.

Sambaza....

Timu ya Taifa ya Cameroon imeendelea na maandalizi kuelekea kwenye mchezo wake wa kufuzu kwenye fainali za Mataifa Afrika dhidi ya Comoros ambao utachezwa Jumamosi ya Machi 23.

Utakuwa ni mchezo wa mwisho wa kundi B na katika kundi hilo tayari Morocco wameshafuzu wakisubiri mshindi katika mchezo huo licha ya Cameroon kuwa na nafasi kubwa ya kufuzu kwani kama watapa sare basi watafuzu lakini kama wakifungwa zaidi ya mabao 3-0 basi Comoros watafuzu.

Rais wa Fecafoot Seidou Mbombo Njoya akiwarambisha mchanga wachezaji wa timu ya Taifa ya Cameroon.

Kumbuka Cameroon ndiye aliyepaswa kuwa mwenyeji wa mashindano ya mwaka huu kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Misri baada ya kamati ya uangalizi ya CAF kugundua kuwa Cameroon hawakufanya maandalizi ya kutosha.

Tuachane na hayo si ndio!!!! Kubwa zaidi nililotaka kukuonesha ni kuwa jana wakati wakifanya mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo, rais wa shirikisho la soka nchini Cameroon Seidou Mbombo Njoya. aliwatembelea wachezaji na kuamua kufanya nao mazoezi.

Hizi ni baadhi ya picha, wanasema ukikiongoza kitu lazima ukijue, na ndio maana kuna watu waliwahi kusema wakati wa uchaguzi mkuu wa TFF ‘Turudishieni Mpira wetu‘.

Rais wa Fecafoot Seidou Mbombo Njoya akiwarambisha mchanga wachezaji wa timu ya Taifa ya Cameroon.
Hapa akiwaelekeza mbinu zake.

Mazoezi hayo yalifanyika jana jioni.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.