Sambaza....

Juhudi za kuendelea kutafuta ndege iliyopotea ambayo ilikuwa imembeba mshambuliaji mpya wa Cardiff City Emiliano Sala zimeanza, baada ya hapo jana kusitishwa.

Ndege hiyo ilipoteza mawasiliano kwenye mkondo wenye visiwa siku ya jana ikiwa imebeba watu wawili ambao miongoni mwao alikuwa ni mshambuliaji mpya wa Cardiff aliyesajiliwa kutoka Nantes ya nchini Ufaransa.

Katika ripoti za leo asubuhi imesemekana kuwa Sala alituma ujumbe wa sauti kwa familia yake kwa njia ya WhatsApp ukiwesema kwamba ‘Ninaogopa sana’ kabla ya ndege hiyo kupoteza mawasiliano.

Wakati huo huo vyombo vya habari nchini Argentina vimeripoti kuwa kuna ujumbe mwingine ambao Sala aliutuma kwa familia yake ukisema kuwa “Nipo katika ndege ambayo inaonekana inakwenda kuanguka,”

Tayari ndege za uokozi tano, pamoja na boti mbele zimejielekeza kuitafuta ndege hiyo kuzunguka sehemu ambayo ilipoteza mawasiliano.

Emiliano Sala mwenye umri wa miaka 28 alikuwa kwenye safari ya kutoka nchini Ufaransa kwenda Wales kwa ajili ya kujiunga na Cardiff ambayo ilimtangaza kumsajili kwa usajili uliovunja rekodi ya klabu wa £15m.

Sambaza....