Wachezaji wa KMC wakishangilia bao katika moja ya mechi za Ligi Kuu ya NBC
Stori

Julio Alivyoiongoza Safari ya Matumaini ya KMC!

Sambaza....

Wakati KMC inatambulisha usajili wake mwanzoni mwa msimu usingeweza kufikiria kama wangehitaji mpaka kucheza michezo ya mtoano “Play off’s” ili kuweza kujihakikishia kubaki Ligi Kuu.

Timu iliyokuwa na mastaa kibao kina Awesu Awesu, Sadala Lipangile, Abdul Hilal, Andrew Vicent, Abdul Hilal, Matheo Anthony na Kelvin Kijiri halafu wakaja kuongezewa kwenye timu kina Ibrahim Ame, Baraka Majogoro, Waziri Jnr, George Makang’a, Daruwesh Saliboko na wengine wengi hukutegemea kwamba ingehitaji kucheza mpaka siku ya mwisho ili kujihakikishia kuwepo katika Ligi ya msimu ujao.

Ilianza Ligi ikicheza na vigogo Simba na Yanga wakipata sare na Simba halafu wakafungwa kwambinde na Yanga lakini ukiutazama mchezo waliounyesha katika mechi hizo kila mtu aliamini msimu huu KMC itafanya vyema na angalau iwe kwenye timu tano bora “top five” ya ligi lakini haikua hivyo.

Ibrahim Ame.

KMC ikaanza kupoteza michezo yake mara kwa mara, kuna wakati ilicheza michezo saba mfululizo bila kupata ushindi wowote. Ilipoteza mchezo tangu December 26 dhidi ya Simba mpaka February 24 dhidi ya Azam Fc kabla ya kuzinduka mbele ya Kagera Sugar March tisa.

Baada ya mambo kwenda ndivyo sivyo April 13 KMC iliachana na kocha wake Hitimana Thiery baada ya kutoka kupoteza mchezo dhidi ya Geita na kumpa timu Jamhuri Kihwelo Julio, kocha wa zamani wa Namungo, Dodoma Jiji na Mwadui.

Wakati Julio anakabidhiwa timu zilikua zimesalia mechi nne na moja ya lengo alilopewa na kuinusuru timu isishuke daraja na angalau ikaangulie kwenye playoffs wakajiulize. Julio alifanikiwa na hatimae timu ikafikia lengo.

Kocha wa KMC Jamhuri Kihwelo Julio akiwa na wachezaji wake mazoezini.

Katika michezo minne hiyo KMC ilishinda miwili dhidi ya Mbeya City na Singida Big Stars halafu wakapoteza miwili pia dhidi ya Dodoma Jiji na Tanzania Prisons na kupelekea kumaliza Ligi wakiwa na alama 30 katika nafasi ya 13.

Baada ya michezo hiyo KMC walicheza michezo miwili ya playoffs dhidi ya Mbeya city na wakiwa chini ya kocha mzoefu Julio walifungwa mbili kwa moja Mbeya na kushinda bao mbili bila jana katika dimba la Uhuru na kuvuka kigingi cha kuteremka daraja.

Akizungumza baada ya mchezo kumalizika msemaji wa KMC Christina Mwagala alisema “Tunawapongeza wachezaji wetu na benchi la ufundi kwa kazi kubwa ambayo wameifanya, haikua kazi nyepesi lakini KMC tumesalia Ligi Kuu.”

Mlinda mlango wa KMC Nurdin Balora akiunyaka mpira wa kona mbele ya washambuliaji wa Mbeya City.

Mwagala pia alitababaisha na kuonyesha kuheshimu mchango mkubwa uliotolewa na Mkurugenzi wa Manispaa, Mstahiki Meya na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

“Tunakwenda kutimiza ndoto ya Mkurugenzi wetu, mama yetu Hanifa Selemani Hamza, Mheshimiwa Mstahiki Meya Songoro Mnyonge na mkuu wa Wilaya Sadi Mtambule kwasababu waliweka mipango madhubuti kuhakikisha kwamba msimu wa 2023-2024 KMC “Kino Boys” inakwenda katika nchi ya ahadi.”

“Tunahitaji tutizmize ndoto za mama yetu, mkurugenzi wetu ambae tangu amekuja amekua akifanya kazi kubwa mno na anaitaka kuifikisha KMC sehemu ambayo hakuna timu nyingine itakwenda kufika. Wana Kinondoni wenye mapenzi mema na klabu muanze kujiandaa kuanzia sasa hivi,” alimaliza Mwagala.

Sambaza....