Blog

Juma Balinya azidi kuwatukana YANGA

Sambaza....

Kwenye maandalizi ya msimu huu kwenye hafla kubwa ya Yanga iliyopewa jina la kubwa kuliko walileta mchezaji ambaye alionekana ni mkubwa kuliko kama mchezaji mpya wa Yanga.

Mchezaji ambaye alikuja Yanga akiwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Uganda akiwa na timu ya Polisi ya Uganda, kwenye mgongo wake jezi yake iliandikwa jina la Juma Balinya.

Mshambuliaji ambaye alitegemewa kufanya makubwa sana akiwa na klabu ya Yanga kwa sababu ya uwezo wake ambao ulionekana mkubwa sana alipotoka.

Lakini cha kusikitisha hakumaliza hata msimu , kwenye dirisha dogo la usajili Juma Balinya aliachwa na klabu ya Yanga, na ile ndoto ya yeye kufanya vyema akiwa na jezi ya Yanga ikawa imeishia hapo.

Leo hii yupo Gormahia FC ya nchini Kenya , inawezekana kabisa kuachwa na klabu ya Yanga kulimuuma na inavyoonekana alikuwa tayari kujitolea kwa ajili ya timu hiyo ya Jangwani.

Juma Balinya anazidi kutuma salamu kwa timu ya Yanga kuwa yeye ni kubwa kuliko Kwani anaendelea kuonesha ukubwa kuliko wake akiwa na jezi ya Gormahia.

Jana Juma Balinya alifunga magoli mawili katika mchezo ambao Gormahia walishinda magoli 3-1 na hii inaonesha ni kama anazidi kuwatukana kwa kutumia miguu yake kuwa hawakuwa sahihi kumuacha.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.