Aishi Manula akiwa langoni mwa Simba
Blog

Kuna kisu kinasogea taratibu kwenye kisogo cha Manula.

Sambaza....

Hakuna sauti inayosikika, na kwa bahati mbaya hata macho hayana uwezo wa kuona. Ila kuna hatua ambazo zinakuja taratibu na kitu pekee kinachoweza kung’amua ni ngozi tu. Ngozi ndicho kiungo pekee kinachohitajika hapa ili kuepukana na hii hatari. Hatari ambayo sitamani itokee na ndiyo maana nafikiria kumkumbusha ili tu aepukana nayo.

Sitamani kumuona akikaa kwenye mbao, natamani sana nimuone akiendelea kusimama kwenye vyuma vitatu vyeupe. Hapa ndipo sehemu pekee ambayo kwa sasa anastahili kukaa. Sitamani kabisa kumuona akikaa kwenye mbao, sitamani kabisa!

Aishi Manula

Yeye ndiye kipa pekee ambaye katika mechi za hatua ya makundi Afcon alikuwa na saves nyingi kuzidi golikipa yoyote yule kwenye mashindano yale ya Afcon.

Kaa chini, tafakari, fikiria jina lolote ambalo unaliona kuwa ni jina la golikipa bora ambaye alikuwepo kwenye michuano hiyo.

Ukimaliza kufikiria nitakuambia kitu kimoja tu, Aishi Manula ndiye kiumbe pekee ambacho kilikuwa na saves nyingi sana kwenye michuano hiyo ya Afcon katika mechi za hatua ya makundi.

Unaona nini ?, naona golikipa tegemeo, golikipa muhimu , golikipa ambaye anaweza kuibeba timu na kuipa alama tatu katika nyakati ngumu ambazo timu inapitia.

-Kaseja

Kipi kinachokuja kichwani kwako unaposikia jina David De Gea ?, bila shaka ni ubora wake wa kuokoa michomo akiwa kwenye lango.

Huyu ndiye kwa misimu ya hivi karibuni amekuwa mchezaji bora na muhimu wa timu ya Manchester United kwa sababu tu alikuwa anaiokoa ipasavyo timu yake.

Alikuwa anaibeba timu katika nyakati ngumu, kuna nyakati timu ilikuwa inaelemewa na kulikuwa na uwezekano wa kufungwa magoli mengi lakini David De Gea ndiye aliyekuwa anasimama imara.

-Beno

Huyu ndiye golikipa muhimu, golikipa ambaye anauwezo mkubwa wa yeye kuibeba timu wakati ambao timu haijui kipi cha kufanya.

Aishi Manula alikuwa anaelekea kwenye hili daraja. Taratibu kuna vitu vinaweza vikaanza kumrudisha asipokuwa makini.

Najua majeraha ni kitu ambacho mchezaji hawezi kukikwepa. Tatizo linakuja pale unapokuwa kwenye majeraha kuna mtu hucheza kwenye nafasi yako.

Nafasi ambayo unaweza usiikute kipindi unapopona. Leo hii Aishi Manula ana majeraha , hali ambayo inatia mashaka kwenye nafasi yake kwenye timu ya taifa na kwenye timu ya Simba.

Kwenye timu ya taifa kuna Juma Kaseja ambaye anaonekana ana njaa kubwa kwa kipindi hiki na kwenye timu ya Simba kuna Beno Kakolanya.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.