Sambaza....

Taarifa hii ni kutoka katika klabu ya Lipuli Fc.

Uongozi wa LIPULI FC unapenda kutoa taarifa kwa wanachama, mashabiki na wapenzi wake juu ya hatma ya mchezaji Asante Kwasi ambaye toka kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu amekuwa mchezaji halali wa LIPULI FC lakini ktk siku za hivi karibuni amezua tafrani kubwa ktk vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu uhalali wake baada ya SIMBA SC kuonesha nia ya kumhitaji.

Kufuatia tafrani hiyo juzi uongozi wa SIMBA SC umeleta rasmi barua kwa uongozi wa LIPULI FC kutaka kupatikana kwa njia bora ya kumaliza sakata la mchezaji huyo na hatimaye wapate ridhaa ya kumtumia kwa mujibu wa taratibu.

Uongozi wa LIPULI FC unakiri kupokea barua yenye ombi la kumtaka mchezaji tajwa hapo juu na kwa kauli moja umeridhia kumaliza sintofahamu hiyo kwa kumruhusu mchezaji Asante Kwasi kwenda SIMBA SC kwa ada ya uhamisho ya kiasi cha shilingi milioni 25.

Kwa msingi huo sasa uongozi unapenda kuwatangazia wanachama, wapenzi na mashabiki wa LIPULI FC ya kuwa mchezaji Asante Kwasi kwa sasa ni mchezaji halali wa SIMBA SC baada ya kukamilisha taratibu zote hitajika.

TUNASHUKURU KWA USHIRIKIANO WENU

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI NA MAHUSIANO LIPULI FC.
23/12/2017.


Sambaza....