Blog

Makosa ya Usajili wa Simba SC (01)

Sambaza....

Tayari Simba imeshawaongeza wachezaji 7 katika kikosi chake kuelekea msimu mpya wa 2020/2021. Kati ya hao kuna washambuliaji wawili, mabeki watatu na Kiungo wawili.

Bila shaka wote tunajua kuwa, Msimu huu Simba itawakilisha nchi katika michuano ya Klabu bingwa Afrika, hivyo hata usajili wake bila shaka unaakisi mashindano haya makubwa barani Afrika.

Sven Vandebroeck

Usajili wa Simba unaonekana kuwa ni wa kimikakati zaidi, hasa kwa kuzingatia ripoti ya mwalimu na madhaifu yaliyojitokeza katika kikosi kwa msimu ujao kuanzia kwenye ligi hadi klabu bingwa Afrika.

Licha ya wadau wengi wa soka nchini  kuusifu usajili huo, kuna walakini kidogo! Walakini ambao unaweza usiifikishe popote Simba katika michuano ya kimataifa.

Uchambuzi huu, umeutazama usajili wa Simba kwa jicho la tatu, hasa jinsi Simba inavyokwenda kupambana kimataifa, hapa utajua Simba wamekosea wapi na ili kusawazisha kosa hilo inawabidi wafanye nini?

Uchambuzi huu utakupa taswira halisi, Simba itakavyocheza kimataifa kwa kuzingatia mifumo ya Sven Vandenbroeck bila kusahau aina ya wapinzani watakao kutana nao.

Narudia, uchambuzi huu hautawalenga Azam, Ihefu au Yanga bali utawalenga Al ahly ya Misri, TP Mazembe, Raja Casablanca, Mamelodi Sundown, zamalek na nyingine nyingi kubwa kubwa kimataifa..hii ni maana tosha kuwa, uchambuzi huu unajikita zaidi kimataifa…

Huko tutachimba tabia za timu kubwa, ni maeneo gani muhimu kwao kupata matokeo na aina ya vikosi walivyonavyo ukilinganisha na kikosi cha Simba msimu huu.

Haya yote tunayafanya ili kuzisaidia timu zetu kufika hatua za mbali zaidi klabu bingwa Afrika na hata kuchukua ubingwa.


Soma zaidi

>


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.